Sunday, November 6, 2011

Zanzibar yashauriwa kuwatumia vyema waatalamu wake

Zanzibar imeshauriwa kuangalia njia za kuwatumia vyema Wataalamu Wazawa walioko nje ya Nchi ili kuharakisha kasi ya Maendeleo ya Jamii .
Ushauri huo umetolewa na Kiongozi wa Wazanzibari waliopo Nchini Marekani ambao wako katika hatua za mwisho kuandaa Jumuiya itakayoitwa Zanzibar Diascora Organization Dr. Omar Haji Ali wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozo Seif Ali Iddi kwenye Hoteli ya Crown Plaza Mjini Washington DC. Nchini marekani.
Dr. Omara alimueleza Balozi Seif kwamba lengo la Jumuiya hiyo ni kuunganisha nguvu kati yao na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuona kwamba uwepo wao nje ya Zanzibar unaleta faida kwa Jamii yote. Alisema hivi sasa wanakamilisha taratibu za kuwaunganisha wenzao wa miji tofauti ili ifikapo Januari mwakani Jumuiya yao ianze kazi rasmi.
“ Tumefanya utafiti na kugundua Wapo Wazanzibari wengi wenye sifa na uwezo mkubwa kitaaluma ambao wanaweza kuitumia na kusaidia nyumbani ”. Alisema Dr. Omar.
Alisisitiza kwamba taratibu zinaandaliwa za akuwaunganisha Wazanzibari wengi walioko katika Jumuiya za Uingereza na Canada kwa ania ya kuwa na kiungo muhimu kati yao na Zanzibar hasa katika maeneo ya Uwekezaji na Uatafiti katika Sekta tafauti.
Alisema kuanzishwa kwa mawasiliano ya moja kwa moja yatatoa fursa kwa wenye nia ya kusaidia kupitia jumuiya hiyo. Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza azma yan Jumuiya hiyo ya Zanzibar Diascora Organization na kuahidi kuipa Baraka.
Balozi Seif alisema Serikali inaunga mkono vikundi vya Diascora na kuvitaka kuwa karibu na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania.
“ Serikali ya SMZ tayari imeshaundan Idara inayosimamia Diascora kwa lengo la kuwaunganisha wazawa walioko nje ya Nchi. Hivyo tutahakikisha mnakuwa na mawasiliano ya karibu na Taasisi hii “ Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Othmana Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment