KUUAWA KWA
MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA (IPC) DAUDI MWANGOSI
Zanzibar
Press Club imepokea kwa masikitiko na hudhuni taarifa ya kifo cha mwandishi wa habari wa
kituo cha Channel Ten ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari
wa Iringa.
Zanzibar
Press Club inaungana na waandishi wa habari wote nchini ambao leo hii
wanatekeleza azimio la jukwaa la Wahariri la kufanya maandamo ya kimya kimya,
kote nchini, kwa lengo la kupinga mauwaji ya aliyekuwa Mwenyekiti Klabu ya
waandishi wa habari wa Iringa, Mrehemu Daudi Mwangosi.
Katika
kutekeleza azimio hilo ZPC imeamuwa kukutana na waandishi wa habari ili kuweza
kueleza kusikitishwa kwao na tukio hilo lilompata mwenzetu wakati akitekeleza
majukumu yake ya kila siku.
Aidha
ZPC inaungana na waandishi na wafanyakazi katika tasnia ya habari nchini, Umoja
wa Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Klabu za waandishi kote nchini, MISA-TAN,
MCT, JUKWAA LA WAHARIRI n.k pamoja na familia ya marehemu Daudi Mwangosi kwenye
kipindi hiki kigumu cha msiba, ambapo
hakuna shaka kwamba tasnia ya habari nchini imelazimika kuingia matatani kutokana
na matumizi mabaya ya nguvu na mabavu ya
Jeshi la Polisi.
ZPC
inalaani kwa nguvu zote mauwaji hayo na yaliyofanywa na watendaji wa taasisi ya
umma pamoja na kutumia nguvu nyingi kupiti kiasi zilizopelekea kifo cha
mwandishi huyo.
Jeshi
la Polisi limekuwa likiendeleza tabia yake ya matumizi ya nguvu kupita kiasi kwa raia wa taifa
hili. Ipo haya ya kutaka kujuwa ni hadi lini jeshi la polisi wataweza
kuimarisha vyema shughuli za ulinzi bila ya kuchukuwa uhai wa mtu?
Hapana
shaka yoyote kwamba kifo cha Daudi Mwangosi kimegubikwa na utata wa kutosha
kuanzi mwazo hadi mwisho wa maisha yake, na hasa ukizingatia kwamba tukio hilo
la mauaji limefanyika hadharani wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Nd.Michael
Kamuhanda alikuwa anatambua uwepo wa Daud Mwangosi na pia umuhimu wa habari hizo kwa taifa, na
kibaya zaidi ni pale kumuona Daud akiwa anafia kwenye mikono ya jeshi la polisi
kulikoni?
Ikumbukwe
kwamba siku zote hata katika vita waandishi wanafanya kazi bega kwa bega na
askari ili kuwajuza wananchi nini kinachotokea na kinachoendelea kwenye uwanja
wa mapambano.
Kutoka
na kifo hicho ZPC inaomba hatua za kisheria zichukuliwe kwa wale wote
waliohusika moja kwa moja na kifo cha mwandishi huyo.
Zanzibar
Press Club kwa saa ingependa kuona utekelezaji mzuri wa kisheria kwa askari
wote ambao walihusika kwenye kadhia hii.
Mbali
na hayo, ZPC inawaomba waandishi wa habari wote wa Zanzibar wawe makini wakati
wanapotekeleza majukumu yao, kwani kutokana na tukio hili limetufanya tuone
kuwa Jeshi la Polisi ni Mdau anayetutia shaka katika utekelezaji wa majukumu
yetu.
Mwenyezi
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amini.
Abdalla
Juma Pandu
Kaimu
Mwenyekiti
Zanzibar
Press Club