Thursday, November 24, 2011

Bara la Afrika limefanikiwa katika kupunguza migogoro kwa kutumia mbunu mwafaka

Changamoto kubwa inayolikabili Bara la Afrika Hivi sasa katika kuelekea kwenye Maendeleo zaidi ni kutumia mbinu na Marifa yaliyopelekea kupunguza migogoro ya Kijamii katika baadhi ya Mataifa ndani ya Bara hili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Viongozi na Wataalamu wanaoshughulikia Kuondosha migogoro Barani Afrika unaofanyika huko katika Hoteli ya Melia iliyopo Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif alisema Jamii ya Kimataifa imeshuhudia utatuzi wa Migogoro kadhaa Barani Afrika hali ambayo kwa kiasi kikubwa imepunguza Migogoro na hata Mauaji ya Raia wasio na hatia. Aliwataka Viongozi na Wataalamu hao kutumia fursa nzuri iliyopo ya Amani iliyorejea Barani humu kwa kuweka Mipango bora itakayoleta faraja zaidi ya ustawi wa Jamii katika miaka ijayo.
“ Tumeshuhudia utulivu wa Kisiasa ilivyorejea ndani ya Bara hili hasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu eneo ambalo Sudan na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo { DRC } zilikuwa katika migogoro mikubwa ya Kisiasa ”. Alikumbusha Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea matumaini yake kwamba Ripoti itakayotolewa na Viongozi hao baada ya kumalizika Mkutano wao itawezesha kujenga mazingira bora ya kudumisha Amani Barani Afrika.
Balozi Seif amezipongeza Taasisi zilizoandaa Mkutano huo ile ya Mwalimu Nyerere, Kituo cha Hali za Binaadamu cha Kimataifa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Norway kwa uamuzi wao wa kufanya Mkutano huo Hapa Zanzibar na hasa ndani ya Jimbo lake ya Kitope.
Alisema uwamuzi wao huo haukuwa wa kubahatisha bali imekuja kwa kuzingatia sifa ya Zanzibar ya amani iliyopelekea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa { GNU } kufuatia Mgogoro wa muda mrefu uliovihusisha Vyama vya CCM na CUF.
Balozi Seif aliwaeleza Washiriki wa Mkutano huo kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inafanya kazi zake vyema huku ikikabiliwa na changa moto kubwa ya kutekeleza matarajio ya Wananchi wote wa Zanzibar.
Akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim alisema yapo Maendeleo makubwa ya kupunguka kwa Migogoro Barani Afrika jambo ambalo limeleta faraja kwao akiitolea mfano nchi ya Sudan.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Haki za Binaadamu bwana David Harland ameipongeza Zanzibar kwa ukarimu wake unaopelekea kupokea Vikao na Mikutano Mzizito ya Kimataifa ndani na nje ya Bara la Afrika.
Wakati wa Mchana akiwa Mkoani Dodoma Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana wa Uongozi wa Kampuni ya uwekezaji vitega uchumi inayojishughulisha na Mradi wa umeme unaotumia upepo na jua kutoka Nchini India.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni hiyo ya Indomount bwana sudhakar amesema Taasisi yake imepanga kutumia Jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni Moja kati ya Bilioni saba zilizotengwa na waziri mkuu wa Nchi hiyo kusaidia Serikali na Taasisi Binafsi Barani Afrika.
Naye Balozi Seif ameuomba Uongozi wa Kampuni hiyo kuangali Meneo ambalo wanaweza kusaidia kati ya yale yaliyoainishwa na kupendekezwa na Zanzibar katika mipango yake ya Maendeleo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment