Tuesday, September 27, 2011

Marehemu Abdulrahman Babu

Marehemu Babu alikuwa jemedari wa mapinduzi ya Zanzibar

Wednesday, September 21, 2011

Muktasari wa Sensei Rumadha Fundi ”Romi”(Sandan)



Rumadha Fundi, “Sensei Romi”Mvuto wangu katika sanaa ya Karate ulianza wakati nilikuwa mdogo mnamo miaka '70s pale Kariakoo,jiji Dar, lakini asili ya kwetu ni Tabora. Kwa bahati nzuri, jirani yetu pale mtaani(Aggrey/Congo) Dar-es-salaam ambako Sensei Bomani alikuwa anakuja kuwafuata baadhi ya wanafunzi wake enzi hizo. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kujua hasa kuhusu Goju Ryu Karate.
Mwaka '78 mwishoni nilipata fursa ya kutembelea “Hekalu la Kujilinda” Zanaki Dojo Kan Shibu, nakuongea na Senpai Magoma Nyamuko Sarya. Kipindi hicho Sensei Bomani alikuwa amekuja toka Marekani na kuja kuwafanyia mitihani wa daraja la “Nidan”kina Senpai Magoma Nyamuko Sarya (Mwafunzi kiongozi), Senpai Tola Sodoinde Malunga, Sensei Gamanya nk. Ndipo nilipoanza shughuli za mafunzo kama”Teenager class”lilijulikana kama (Bomani Brigade)
Baada ya mtiani wa mkanda wa kahawia '81, kiongozi wetu (Senpai Magoma) aliondoka kwenda India na Phillippines kusomea sanaa mbalimbali na Yoga , ndipo na mimi nikajiunga nae huko India na baadae kwenda Sweden mnamo mwaka wa '85 katika shule ya Yoga”Internation school of Intution Practice” au katika lugha ya Sanskrit ambayo ndio inatumiwa na Yoga hujulikana kama “Prakshimata - Ananda Nilayam” huko, Gullringen, Vimmerby, Sweden.
Hapo ndipo lipohitimu ualimu wa Yoga baada ya kozi ya miaka miwili na kurudi tena Calcutta, India kwa Master mkuu wa Yoga duniani na hatimae kupata ngazi ya juu katika mafunzo ya Yoga mnamo mwaka wa '90 “Avadhuta”.
Vile vile nilipata fursa ya kwenda Houston, Texas mwaka '88 na kuendelea na mafunzo ya Karate mtindo wa “Okinawa Goju Ryu” chini ya uongozi wa Master Sensei Morio Higaona mwenye Dan 10, kiongozi mkuu wa “International Okinawan Goju Ryu Karate -Do Federation” na kupata fursa ya kupata daraja la kwanza '89 toka kwa Master Higaona huko Tampico, Mexico chini ya uongozi wa Sensei Mario Falcone wa Mexico na Sensei Ramon Veras wa Houston, Texas. Hawa ni moja ya walimu walio nisaidia kwa dhati katika sanaa ya Karate. Ninapenda kutowa shukran nyingi kwa walimu wote ambao waliweza kunifundisha sanaa hii sehemu zote zile nilizoweza kushiriki katika fani hii kama vile, Master Morio Higaona, Master Teruo Chinen, Sensei kiongozi wa Okinawa Goju Ryu, in Okinawa, Sensei Matsuda, na Sensei Muramatsu.Hao wote ni viongozi wa ngazi za juu sana duania katika sanaa ya mtindo wa Goju.
Kwa sasa hivi nina daraja la tatu “Sandan”mkanda mweusi kwa muda mrefu sasa. Kumbu kumbu yangu kubwa ni kuwa na ushirikiano mwema na wanafunzi wengi wa zamani pale “Hekalu la Kujilinda” ambao sasa hivi bado wapo mbele katika kusaidia vijana kama Sensei Maulid Pambwe, Rashid Almas, Mohamed Murudker, Wilfred Melkia, Geofrey Sawayael “Shoo”, Mbezi, Metthew huko Mwanza, Ndaukile,Edgar Kaliboti huko Sidney Australia, Salum Kitwana Khamisi huko UK. Hata wale wote ambao nimewasahau popote pale duniani.
Pia, natoa shukran nyingi sana kwa mtu muhimu sana katika maisha yangu ya kisaa ya Karate na Yoga ambaye ulikuwa ndio mashine ya mafanikio yangu ngazi zote hizo, Senpai Magoma Nyamuko Sarya(Mahadev/Mrnal) popote pale alipo nasema,”Shkran”.
Mipango ya uendelezaji sanaa hii kwa miaka ya mbele huko Tanzania ni muhimu sana. Moja ya hiyo mipango ni siku moja kufungua chuo cha sanaa ya kujilinda na kutumia nyezo za Karate”Kobudo” Kama vile “Sai, Tonfa, Nunchaku,Bo, Shuri, “Three section Nunchaku” nk. Kwa ajili ya kufundisha Tanzania. Ingawa sio leo wala kesho, bali ni moja ya mipango ya mbele huko katika maisha nitaporudi Tanzania, nakuwashirikisha walimu wengine wenye uzoefu mwingi katika kutumia nyenzo hizo.

PRESS RELEASE

Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya migodi Afrika { AFRICA BARICK GOLD } inakusudia kuandaa ampango wa kusaidia vifaa vya uokozi kwa vyombo vya usafiri wa baharini kwa lengo la kupunguza maafa wakati zinapotokea ajali baharini.
Mjumbe wa Bodi hiyo Balozi Bakari Mwapachu ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha salamu za rambi rambi kwa mweyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Balozi bakari Mwapachu amesema utafiti unaonyesha kwamba vyombo vingi vya usafiri wa baharini haviwezi kutosheleza vifaa vya uokozi wakati vinapopatwa na ajali.
Amesem Uongozi wa Bodi hiyo utaandaa utaratibu wa kuzungumza na Taasisi na Mamlaka zinazosimamia usafiri wa baharini ili kuona mpango huo unaanza kutekelezwa ambapo utahusisha pia na vyombo vidogo vidogo vya uvuvi.
Balozi Mwapachu ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga Hoja kwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Afrika Mashariki kwa kuishauri iangalie mazingira ya kujenga kituo cha Mawasiliano Hapa Zanzibar. Bodi hiyo imetowa mkono wa pole kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia shilingi Milioni 60,000,000/-,
Taasisi nyengine zilizochangia mfuko wa maafa ni kampuni ya Elewana Afrika inayoendesha Biashara ya Hoteli Tanzania pamoja na Uongozi wa chama cha NCCR Mageuzi .
Mweyekiti wa Chama hicho Bwana James Fransis Mbatia amesema changamoto iliyopo ni watu wote wenye mapenzi na janga hili wanaongeza ushirikiano katika kusaidia kukamilisha kutatua tatizo hili.
Akipokea michango hiyo Mwenyekiti Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif ameendelea kuzisukuru Taasisi na jumuiya zilizojitolea kusaidia tatizo hili la maafa ya kuzama kwa meli Zanzibar.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Wednesday, September 14, 2011

UN pays tribute to the victims of Zanzibar boat accident

The United Nations System in Tanzania observed a minute of silence on Monday this week in remembrance of the victims of the boat that capsized off the coast of Zanzibar on early morning Saturday, September10th.
At an emergency Town Hall meeting called for at the UN Compound, the United Nations Resident Coordinator Alberic Kacou told UN staff in Dar es Salaam that immediately after hearing news on the disaster, the UN provided assistance in the form of blankets, gloves, water and high-calorie biscuits for the survivors.
He also noted that all UN staff stationed in Zanzibar have been accounted for as being safe although some have lost family members and are highly traumatized by the tragedy.
“A UN counselor has been sent to Zanzibar to provide post traumatic counseling to our colleagues. She reports that the situation is very difficult,” Kacou said. The Resident Coordinator affirmed that the UN is working hand in hand with the government in dealing with the situation.
On his part, the UN Secretary-General Ban Ki- Moon has sent condolences to the Government and people of the United Republic of Tanzania and Zanzibar and the families of the victims.
The Secretary-General said he is “profoundly saddened by the tragic loss of life” and “wishes a speedy recovery to the people who survived the accident.”
“The United Nations stands together with the people of Tanzania at this tragic moment,” said the UN Secretary General.
The sunken boat christened MV Spice Islander was heading to the island of Pemba from Zanzibar when it capsized in the wee hours of Saturday morning near Nungwi Village. Many lives have been lost. Following the incident the Government announced three days of mourning during which the national flag will be flown at half mast countrywide.
At the advisory services level, the activities consisted in:
-The UNDP assisted the department of Disaster Management (DMD) to organize and coordinate the response through the UNV placed in that office.
-The WHO team joined the team of the Ministry of Health Senior officials to provide advises on the organization of the emergency management at the main hospital.
-A UNICEF team assisted the Hospital for the “Prise en charge” of the children together with Save the Children.
-The UN stress advisor and counselor undertook collective debriefings and counseling with rescue teams to anticipate on eventual Post Traumatic Stress Disorder (PTSD) syndromes, specifically with teams having dealt with women, children and dead bodies management.
On the material support, the UN provided through different UN agencies respective contribution:
Logistics - shelter
.Tents and tarpaulins (200mx1) used on the three sites
General supply & Medical
• 52 boxes of biscuits (Nungwi & Mnazi Moja)
• 500 blankets (200 Unguja & 300 Pemba)
• 1680 Bottles of water for the rescue workers and survivors
• 50 boxes of IV fluids
• 100 boxes of Canula
• 200 rolls of plaster
• 200 rolls of Cotton wool
• 10 litres of Methylated Spirit

Hizb ut-tahriri rambi rambi rambi

HIZB UT-TAHRIR AFRIKA MASHARIKI YATOA RAMBI RAMBI KWA MSIBA WA KUZAMA KWA MELI.
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki imepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya kuzama kwa meli ya Spice Islander iliyotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 10/09/2011 katika eneo la mkondo wa Nungwi baina ya kisiwa cha Pemba na Unguja, na tunaungana na walioathirika kuwafariji kwa msiba huu na kuwataka wawe na subra katika kipindi hiki kigumu.
Aidha, tunatangaza kwa ulimwengu wa kiislamu kwamba una wajibu kwa haraka kusaidia katika uokozi na kuzisaidia familia zilizopotelewa na ndugu ambao ni nguvu kazi ya familia hizo.
Ajali hii ni kielelezo wazi ziada cha kushindwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutoa usafiri wa uhakika baina ya kisiwa cha Unguja na Pemba pia kushindwa kwa mamlaka zake
husika kusimamia vyema usalama wa abiria na uokozi.
Wakati Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki tukiwafariji kwa subra na ustahamilivu wote
walioathirika, pia tunatamka wazi kwamba ni dola ya kiislamu ya Khilafah pekee ndio yenye dhamira ya kweli na ya kimaumbile katika kulinda na kuokoa maisha ya watu.
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

Tuesday, September 13, 2011

Mola awape Subra wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha Msiba!


Na Ramadhan Himid, Zanzibar
Mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa juu ya msiba mkubwa uliolikumba taifa huko Zanzibar katika usiku wa kuamkia tarehe 10 Septemba mwaka huu wakati Meli ya MV Spice Islander iliyokuwa ikitokea Zanzibar kuelekea Wete Pemba kuzama katika mkondo wa Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wale wenye imani inayofanana na mimi huwa kila tunapopatwa na jambo zito kama hili hulielekeza moja kwa moja kwa Mola wetu kwa kusema “Inalillah Waina iraih rajiuun”, yaani, “Sisi sote ni Waja wa Mungu na kwake yeye tu ndio Marejeo”.
Bila shaka lililoandikwa na Mungu halipanguki, na tukiamini hilo tutakubaliana pia kwamba sisi tuliwapenda sana jamaa zetu ila Mungu amewapenda zaidi, na yeye tu pekee ndiye mwenye maamuzi sahihi ya kufanya apendavyo.
Sina lengo la kukumbusha kilio matangani, lakini msiba huu ni mkubwa na umemgusa kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyengine na ndio maana tunasema ni msiba wa kitaifa ambapo nami kupitia kalamu yangu hii sinabudi kutoa rambi rambi yangu kwa ndugu zetu tuliowapoteza
Kwa hakika Zanzibar nzima ilijinamia na haikuwa rahisi mtu kujizuia hisia zake na watu walikuwa na kila sababu ya kuangua vilio vyao na hata kushindwa kula.Tunasema ni msiba mkubwa haujawahi kutokea , na tumuombe Mungu atuepushe kwa hili na jengine.Amin.
Mungu atupe subra katika kipindi hiki kigumu kwa kuwapoteza jamaa zetu 197 ambao walifariki dunia na 619 waliookolewa. Ni kipindi kigumu lakini kwa kuwa mwanadamu amepewa sahau, inshaallah Mungu atatupa lenye kheir na sisi zaidi ya hao tuliowapoteza.
Ajali hii mbali na kutukumbusha ajali ya Mv Bukoba iliyotokea Tanzania Bara, bali pia inatukumbusha kuwa ni takribani miaka miwili hivi ambapo MV Fatih ilizama chini ya Bandari Zanzibar May 27, 2009 ambapo tuliwapoteza watu saba.
Mbaya zaidi kinacholeta taharuki kwa ajali hii ya MV Spice Islander ni kwamba idadi halisi haijulikani hadi sasa kwani inasemekana meli hiyo ilisheheni pomoni kuliko uwezo wake wa kawaida huku ikiwa na tani nyingi za mizigo.
Idadi ya waliokata tiketi inasemekana ni 610 lakini hofu ni kwamba majeruhi waliopatikana ni 619 na waliopatikana wamefariki ni 197, ni sawa na 816. Lakini ukifuatilia kwa karibu watu wengi bado wanaendelea kuwatafuta jamaa zao ambao walikuwemo katika meli hiyo, tena wengine wakiwa na watu watano ama zaidi, hebu na tujiulize meli hiyo ilikuwa na abiria wangapi?
Hili ni swali zito ambalo kila mmoja wetu anaweza kuwa na jawabu yake mwenyewe, lakini ni vyema wenye vyombo vya usafiri wa majini pamoja na Mamlaka husika kila mmoja akatekeleza wajibu wake kwa kuweka mbele maslahi ya umma kuliko maslahi yao binafsi. Umefika wakati kuhakikisha kwamba kunakuwepo kwa usimamizi wa karibu wa kuhakikisha kila meli inakuwa na idadi maalum ya abiria na inapakia kadri ya uwezo wake, tuache tabia ya kujali kitu kuliko utu.
Ni vyema pia zikawapo kumbukumbu maalum za wasafiri jambo hili litasaidia sana kujua idadi halisi kuliko kuzusha taharuki mitaani kama ilivyo hivi sasa ambapo kila mmoja anasema vyake.Jambo hili si gumu iwapo kila mmoja atatekeleza wajibu wake ipasavyo kwa kujali uzalendo na uchungu wa nchi yake. Aidha umefika wakati kwa Mamlaka husika kutoa taaluma ya wajibu wa msafiri na haki zake akiwa safarini pamoja na wajibu wa mwenye chombo na wafanyakazi wake aliowaajiri wakiwa wao ndio hasa dhamana wa chombo hivyo wakati wa safari.
Ninalisema hili kwasababu maalum, kwanza inasemekana kuwa chombo hicho kilijaza kupita kiasi na kabla ya kuondoka bandarini hapo kilikuwa tayari kimeshalemewa upande mmoja na hadi baadhi ya waliokata tiketi kuahirisha kusafiri kwa siku hiyo, lakini kwanini wafanyakazi wa chombo hicho nao wakashindwa kutimiza wajibu wao kwa kupunguza ama mizigo au abiria badala tu ya kuruhusu kuondoka bandarini ilhali wanajuwa kuwa lolote linaweza kutokea.
Kwa upande wa abiria, naamini walijua kuwa chombo kilijaza kadri ya uwezo wao lakini nao kama binadamu huwa hawapewi haki zao kama wasafiri na hii pia inatokea hata kwa usafiri wa nchi kavu abiri wanapodai kuwa chombo kinaenda mbio hutishiwa kuteremshwa njiani ama ndio dereva akakasirika na kuondeza mwendo zaidi.Ndio maana nikasema taaluma hii izidi kutolewa kuelezea haki na wajibu wa msafiri na msafirishaji wakati wa safari.
Tukishindwa kuyafanya haya kwa kuamini tu kuwa mwenye sukani ndiyo mwenye uamuzi wa kufanya atakavyo, tunaweza tukaharibikiwa mno, lakini kama tutakuwa na utaratibu maalum wa kuwajibishana kati ya mwenye chombo kuhakikisha kuwa chombo chake kinakuwa kizima, dereva (kapteni, rubani, baharia) anajali maisha ya aliowapakia na abiria kujua haki zake kutonyamazia kasoro ambazo zinaweza kupoteza uhai wake ….hapo tutakuwa salama!
Waswahili wanasema “ukupigao ndio ukufunzao”,ni wakati mwafaka hivi sasa kuwa na vyombo vya kisasa vya usafiri pamoja na kuokolea pindipo kutatokea maafa makubwa kama haya,Mungu atuepushie.
Serikali yetu nayo lazima iweke kipaumbele cha pekee kwa kuhakikisha kwamba tunakuwa na vyombo vya kisasa vya usafiri wa majini, kwani wengi wetu tunategemea usafiri wa bahari ambao ndio nafuu kuliko usafiri wa anga kwa safari za kwenda Pemba na Dare-es-Salaam , hasa ikizingatiwa kuwa hakuna usafiri mwengine mbadala kutokana na visiwa vyetu kuzungukwa na bahari.
Kwa kweli taifa limepoteza rasilimali muhimu sana kwa uzembe tu wa watu fulani ,inasikitisha na inauma sana kuona watu wengi wamefariki katika ajali hiyo , hasa wakiwemo wanawake na watoto.
Tuiachie Tume ya Usalama wa Taifa fanye kazi yake, lakini haki lazima itendeke na kusiwepo upendeleo kwa kuwafumbia macho baadhi ya watu ambao tukiendelea kuwafumbia macho kuna siku watatufumbua macho huku tumekufa.

Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu maiti zilizookotwa Mombasa

PRESS RELEASE
Maiti tano zinazofikiriwa kuwemo kwenye meli ya m.v spice zimeokotwa katika ufukwe wa mombasa nchini Kenya. Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya maafa zanzibar Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi seif ali iddi ameeleza hayo afisini kwake vuga wakati akiendelea kupokea salamu za pole kutoka kwa wawakilishi wa taasisi na jumuiya mbali mbali waliofika fasini hapo kuwafariji.
Balozi seif amesema taarifa hizo zimekuja kufuatia mawasiliano kati ya serikali na Afisi ya ubalozi mdogo wa Tanzania uliopo mombasa nchini Kenya. Amesema maiti hizo tano zinafanya idadi ya maiti waliopatikana hadi sasa kufikia 202.
Makamu wa pili wa rais amezishukuru taasisi zote zilizotoa mchango wao ambao unaashiriia kukugwa na msiba huo.
Taasisi zilizowasilisha ubani wao ni pamoja na chama cha mapinduzi CCM makao makuu,wabunge wanawake wa bunge la afrika mashariki,jumuiya ya khoja shia isnashir ya afrika, uongozi wa baraza la wawakilishi Zanzibar,arusha wazee club, benki ya NMB kwa kusirikiana na baraza la manispaa Zanzibar pamoja na benki ya vitega uchumi Tanzania { TIB } pamoja na Kampuni ya IPP Media ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd amepokea michango kutoka taasisi tofauti zilizohamasika kuchangia familia zilizopatwa na maafa hayo.Waliochangia fimilia hizo ni pamoja na jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Zanzibar{ zapha + }, Taasisi ya uwekezaji vitega uchumi Zanzibar { ZIPA }, Jumuiya ya Wanasheria Zanzibar
{ Zanzibar law Society }, Taasisi ya Huduma za Viwanja vya Ndege Tanzania { ceo }.
Akitoa shukrani zake Waziri Aboud amesema kwamba nia ya Serikali ni kuona kuendelea kuwatafuta watu wote ambao bado hawajapatikana kufuatia ajali hiyo.
Wakitoa salamu zao za pole wawakilishi wa Taasisi hizo wameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuleta Heshima ya nchi kutokana na kukabiliana vyema na maafa hayo kwa Ushirikiano wao wa karibu na Wananchi na Taasisi za Uokozi. Jumla ya shilingi la Kitanzania milioni148,200,000/- zimepokelewa kutoka kwa Taasisi na Jumuiya tofauti za ndani na nje ya nchi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Monday, September 12, 2011

September 11,2011

Statement attributable to the Spokesperson for the UN Secretary-General on the Zanzibar, Tanzania ferry disaster.

The Secretary-General is profoundly saddened by the tragic loss of life after a ferry capsized off the coast of Zanzibar, United Republic of Tanzania, on 10 September.

He expresses his condolences to the Government and people of the United Republic of Tanzania and Zanzibar and the families of the victims. He also wishes a speedy recovery to the people who survived the accident.

The United Nations stands together with the people of Tanzania at this tragic moment.

Sunday, September 11, 2011

Method Kilaini ndani ya KCP

MKUTANO MKUU WA KAGERA PRESS CLUB (KPC) Septemba 10, 20
PONGEZI
Kwanza ya yote napenda kuwashukuru kwa heshima ya kunialika niwe mgeni rasmi katika mkutano wenu huu mkuu. Waandishi wa habari ni sehemu muhimu katika jamii na mhimili wa nne wa jamii. Hivyo napenda kuwapongeza kwamba mliamua kuunda chombo kinachowaunganisha katika kutimiza majukumu yenu makubwa ya kuunda jumuiya na jamii ya watu kwa kuwapa habari, kuwaelimisha, kuwahamasisha na kuwapa changamoto. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Kwa watu wa habari ni rahisi kujikuta wanararuana na kuharibiana kazi badala ya kuungana katika kutoa mema kwa watu bila kukwaza ukweli.
UMUHIMU WA WAADISHI WA HABA
1. Waandishi wa habari na vyombo vyao wana uwezo wa kujenga au kuharibu kwa sababu ndio wnaotoa habari za matukio na watu wanawaamini sana. Tajiri mmoja mmiliki wa gazeti alishindwa kumwaminisha mfanyakazi wake juu ya habari Fulani lakini alipoiweka katika gazeti lake mfanyakazi huyo alikuwa wa kwanza kmumwambia kumbe ni kweli kwa sababu ameviona gazetini. Kuposha habari huleta madhara makubwa kwa jamii.
2. Waandishi wa habari wana uwezo wa kuchokoza hata viongozi wa serikali na kuwafanya watimize wajibu wao. Mnakumbuka sakata la magogo ya miti kutoka Rufiji yaliyosafirishwa kwa wingi hata misitu ikaanza kutoweka, vilikuwa vyombo vya habari vilivyopuliza filimbi na hatua zikachululiwa. Huu ni mfano mmoja kati ya matukio mengi.
3. Vyombo vya habari vinatoa mwanya kwa watu kutoa maoni yao na kufanya sauti ya watu hata wale wanyonge isikike. Sauti ya wasio na sauti.
MAADILI YA WAANDISHI WA HABARI
Inafurahisha kuona kwamba KPC ni wanachama hai na wenye uhusiano mzuri na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Baraza hili lina kazi siyo tu ya kutetea uhuru wa habari kufuatana na ibara ya 18 ta katiba ya Tanzania, lakini vile vile kuhakikisha wanahabari wanafuata maadili ya kazi yao. Ili kukuza heshima ya fani yenu hapa Kagera inabidi muwe wanachama hai kwa matendo katika baraza hilo. Uandishi wa habari bila maadili ni sumu kwa jamii. Mifano mikubwa ni jinsi vyombo vya habari vilivyotumiwa Rwanda na Kenya wakati wa machafuko na mauaji.
Jukumu la mwanahabari ni kutoa ukweli hata ule mchungu kwa ajili ya kujenga na kutibu jamii, kuleta uelewano na siyo chuki, mshikamano na siyo utengano, kujenga na siyo kubomoa. Hiyo kazi mtaifanya kama mtasaidiana kufuatana na maadili yanayotolewa na baraza hilo ambalo ni la hiari, huru na lisilo la kiserikali lililoanzishwa mwaka 1997, likiwa na lengo la kujirekebisha lenyewe ili lisitoe mwanya na sababu kwa wengine ikiwemo serikali kuwabana kwa kisingizio cha utovu wa nidhamu. Muwe na uwezo wa kukosoana na kuambizana ukweli.
UHITAJI WA WANAHABARI MKOANI KAGERA
Mkoa wa Kagera una uhitaji wa kupata wanahabari wengi na makini. Kuna watu wengi nje ya mkoa hasa wanakagera amabao wana kui kikubwa kupata habari za Kagera. Hivyo lengo lenu la kuitangaza ni zuri na lenye tija kwa sisi sote. KPC ina kazi kubwa na nzuri ya kuwasaidia na kuwahamasisha wanahabari wa mkoa wa Kagera kutimiza majukumu yao ya:
a. Kutangaza mambo mengi mazuri yanayofanywa Kagera kwa wanakagera na ulimwengu mzima. Ni ninyi mtaweka Kagera kwenye ramani ili mtu asiulize Kagera ni nini? Mnategemewa kuienzi na kuiuza Kagera, utajiri wa kitalii, mazao yake mazuri, utamaduni wake na mafanikio yake. Ninyi muwe wa kwanza kujifunza na kujua Kagera na utajili wake. Tembeleeni sehemu mbali mbali na kutaneni na watu mbali mbali.
b. Kurahisisha kuomba misaada kwa ajili ya Kagera wakati wa shida na maafa kwa kuyatangaza. Mfano ni kimbunga kilichopiga Muleba. Ilituwia rahisi kuomba misaada nje kwa sababu taarifa ilitoka kwenye vyombo vya habari na hatukupashwa kutoa maelezo mengi. Hivyo juzi nilikwenda huko kugawa mabati na mashuka kutoka Caritas Tanzania kwa niaba ya kanisa Katoliki, ninawashukuru sana.
c. Kusisimua viongozi mara nyingine kutoka usingizini kwa kuyaainisha matatizo ambayo hawajayafanyia kazi. Kazi yenu siyo kila mara kufuatana nyuma ya viongozi na kuripoti majigambo yao na kuwafurahisha, nendeni na kule amabako wamesahau na kuonyesha uozo uliopo. Msiogope, mwandishi wa habari anayeogopa na kuwa kibaraka mradi kula hatakuwa hata siku moja mwandishi makini mwenye kuheshimiwa. Fichueni uozo, uzembe na hata ufisadi kama upo hapa Kagera na hapo vitafanyiwa kazi.
d. KPC iwe shule kwa ajili ya waandishi wadogo ambao bado hawajapata elimu kubwa ya uandishi ili waweze kuleta habari kutoka vijijini. Nashukuru na hongera nma uhusiano mzuri na (MCT) na Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) na mmefanya kwa mafaniko mradi mkubwa nao, na wao wako tayari kuendelea nanyi. Hivyo hakikisha wale mtakaowachagua wawe na uwezao wa kuendeleza juhudi hizo.
e. Chama kitoe msaada kwa magazeti na vyombo vya habari vya hapa mkoani Kagera na kuanzisha vingine. Najua wengi kula yao ni magazeti na vyombo vya habari vya jijini Dar es Salaam na Mwanza na sina ugomvi nal kwa sababu na linatusaidia kupeleka habari na maoni yetu taifani. Lakini ujuzi wenu usaidie vile vile vyombo vya matumizi ya ndani ili Bukoba/Kagera iwe kituo cha habari (hub).
f. Vyombo vyetu vya habari viwe uwanja wa wanachi kuleta maoni, mawazo, furaha, manunguniko na mafaniko yao kwa umma. Nafurahi sana kusikiliza redio zetu.
g. Changamoto moja ni kwamba waandishi wa habari wengi wako hapa Bukoba mjini na wilaya nyingine hazina hata mmoja. Nilikuwa Muleba Mkuu wa wilaya akaniambia kule hakuna mwandishi hata mmoja, nikashangaa. Najua ninyi hamtahamia Muleba lakini mnaweza kuwahamasisha wana Muleba walu wachache wakajihusisha na uandishi wa habari hata kama siyo wataalamu wakubwa nanyi mkahariri habari hizo. Vile vile haitoshu ninyi kuandika habari za Dar es salaam tu na labda kidogo za Bukoba mjini hasa wanapotembelea viongozi wa juu bali fanya utafiti juu ya sehemu zote za Kagera.
WANAHABARI KAMA FAMILIA MOJA
Inajulikana kwamba magazeti na vyombo vya habari vina wenyewe na kila mwenye chombo ana lengo lake. Mwandishi au mtangazaji lazima afuate sera ya mwenye chombo na vingine vinapingana katika mielekeo yao. Kwetu hilo siyo baya kwa sababu linatupa sisi wadau mitazamo tofauti ili nasi tuweze pupambanua kati ya pumba na mchele. Licha ya hilo ninyi wanahabari mnapashwa kuwa marafiki na ndugu bila uhasama ingawa mara nyingine mnapingana katika maandishi yenu mradi usiseme uongo bali iwe tu ni mitazamo na mkazo tofauti katika ukweli huo huo.
Mkiwa familia moja hapo mipango yenu ya maendeleo itafanikiwa. Leo uko gazeti/radio/TV ya mlengo wa kulia, kesho utakuwa na lile la mlengo wa kushoto bali wewe ubaki mwanahabari. Pawepo uwezekano wa kuketi na kuchambua pamoja habari ndani na nje ya vyombo vya habari ili kupanua ugo wenu. Kuwa na miradi ya pamoja kama vyombo vya habari, mini press na hata SACCOS ya kujikimu. Mwanahabari mwenye njaa husaliti fani yake kwa sababu hulipwa kupindisha habari ambacho ni mwiko na aibu kwa manahabari na madhara yake ni makubwa kwake binafsi na kwa jamii.
Ni vizuri sana kwamba mnaweka mazingira kwa wale wadogo kufanya kazi kama kuwapa kamera, scanner, computer, printer vya kuandikia stori zao na mengine. Kupitia hapo watajifunza na kukua kuwa wanahabari wanaojitegemea.
Uanachama siyo tu kupata faida lakini vile vile una majukumu yake. Mafanikio hutokana na jasho na juhudi. Ukiwa mwanachama kwa mfano itabidi ulipe ada yako mapema ili chama kimudu kazi zake, ushiriki katika mikutano inapoitwa, uchangie kwa namna mbali mbali kwa hali na mali. Asiyetupa haokoti, tupa kwanza na hapo utaokota mengi. Uwajibike, mkipata mradi wa kutekeleza, usaide kuutekeleza vizuri na kutoa ripoti zote zinazohitajika kwa wakati ili waweze kuwaamini na kuwapa miradi mingine. Usiganganie marupurupu ya miradi bila kuitolea jasho lako. Asiyefanya kazi asile.
UCHAGUZI
Mimi simpigii ye yote kampeni na wala sijui nani anagombea, ila nawaombea uchaguzi wenye tija na uwaweke viongozi waostahili na wenye sifa katika safu za kutoa maamuzi. Wawe viongozi wabunifu wataoimarisha siyo tu vilivyopo bali watabuni na njia nyingine za kukiendeleza chama na fani ya uandishi Kagera kwa ujumla. Wawe viogozi wawajibikaji na waaminifu wataoaminiwa siyo tu nanyi lakini hasa wafadhili wa nje ili misaada inayotolewa ifikie lengo lake kwa wakati na kwa mafanikio. Viongozi wa heshima na ustaarabu ambao wataheshimiwa na wote hata viongozi wa serikali na taasisi nyingine ili wawe na uwezo wa kuwasilana nao bila shida. Viongozi wenye kujali kiasi kwamba wataweza kuwasiaidia vijana wanaotaka kuingia fani hii lakini hawajui waanzie wapi au wameingia lakini bado wanyonge bila kuwadhalilisha, kuwakandamiza au kuwaomba hongo.
Ndugu mwenyekiti napenda kumalizia kwa kuwatakia kila la heri na fanaka katika mkutano wenu mkuu ambao utatoa vingongozi bora wa kusimamia fani hii muhimu katika kipindi kijach cha miaka mitatu hapa Kagera. Sisi tuko pamoja nanyi.
Mwenyezi Mungu awabariki
+Method Kilaini
Askofu Msaidizi
Jimbo Katoliki la Bukoba

Sunday, September 4, 2011

Taarifa kwa vyombo vya habari

PRESS RELEASE
Ujenzi wa Afisi za Wabunge ndani ya Majimbo ni uamuzi sahihi wa Bunge La Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha huduma za Wananchi zinapatikana kwa haraka muda wote. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope amesema hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa Afisi ya Jimbo hilo baada ya kukamilika Ujenzi wake.
Hati za Makabidhiano ya Afisi hiyo ya Mbunge wa Kitope imetiwa saini kati ya mbunge huyo Balozi Seif na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Nd. Vuai Ali Vuai ambapo ujenzi wa Afisi za Wabunge unasimamia na Afisi za Wakuu wa Wilaya. Akikabidhi hati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kakaskazini B Nd. Vuai Ali Vuai amesema ujenzi huo unafuatia azimio la bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wa kujenga Afisi za Wabunge Majimboni.
Akipokea Afisi hiyo mbunge wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi amewahakikishia wananchi hao kwamba yeye na mwakilishi wa Jimbo hilo Mh. Makame Mshimba wataendelea kushirikiana na Wananchi hao ili Maendeleo ya haraka ndani ya Jimbo hilo yafikiwe. Wakati huo huo Balozi Seif Ali Iddi ameutembelea ushirika wa mwendo wa jongoo wa Kazole ambao unajishughulisha na ukulima wa mboga mboga.
Akiunga mkono juhudi za wanaushirika hao Balozi Seif Amekabidhi ndondo kwa kuendeleza ujenzi wa Afisi ya Tawi la CCM la Kijiji hicho pamoja na mpira wa Maji na vifaa vyake na kuahidi kutoa makalbi ya kisima ili kuwaondoshea shida ya upatikanaji wa maji katika mradi wao wa kilimo.
Balozi Seif pia amekabidhi msaada wa Matofali, Saruji, mchanga na fedha za fundi kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Tawi la CCM La Kichungwani na kushauri ni vyema Tawi hilo likaanza kutoa huduma mwaka ujao. Vifaa na msaada huo kwa Kikundi cha Ushirika cha Uwendo wa Jongoo na Afisi za CCM vimegharimu Shilingi Milioni Moja Nukta Moja.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Thursday, September 1, 2011

Edd Mubarak




Je unamfahamu Meneja wa Mtegani?

Bw.Saumu Ali ndie Meneja mkuu wa Megani radio Fm, wakati huu ni mwandishiwa wa habari wa mkoa wa kusini Unguja
Meneja Saumu akibadilishana mawazo na mjumbe wake

Kazi ipo

Bi Rose mwenye baibui, kutoka UN Women wakati alipotembelea Mtegani radio hivi karibuni



Na hivi ndivyo radio yetu inavyofanya kazi na ndio maana tunataka msaada wake wa hali na mali na hasa katika suala zima la vifaa

Radio itumiayo juwa (solar power)

Radio ambayo inaonekama kama vile imetupwa lakini ukweli haikutupwa bali imewekwa juani kwa ajili ya kupata chaji ya kuweza kufanya kazi


Mtegani radio family

Baba na watoto wake ambao ndio wanaofanya timu nzima ya matangazo ya radio Mtegani Fm 91.9 Mkunduchi-ZanzibarHawa ni miongoni mwa kamati ya uongozi ya radio Mtegani pamoja na watangazaji, fundi mitambo, DJ pamoja na viongozi kutoka UN Women Dar-es-salaamHii ndio timu kamili ya matangazo ya mtegani fm Zanzibar