Friday, November 4, 2011

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yassaini mkataba wa mashirikiano katia yake na chuo cha ufundi cha Florida

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba wa Mashirikiana kati yake na Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida { FAMUJ } Nchini marekani.
Mkataba huo una lengo la kubadilishana uzoefu na Utaalamu kati ya chuo hicho na chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZAZ}.
Utiaji saini huo umefanyika katika Majengo ya Chuo hichocha Florida yaliyopo katika mji wa Tallahassee ambapo kwa upande wa Zanzibar umewakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Florida umewakilishwa na Rais wa Chuo hicho cha
{ FAMU } Dr. James ammons.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa pia na wanafunzi wa fani fofauti chuoni hapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri taaluma inayotolewa na chuo kikuu cha Florida iingie katika nchi changa ili kuleta mabadiliko ya kilimo na ufundi.
Balozi Seif alisema Mataifa mengi yanayoendelea hasa yale ya Bara la Afrika bado yanashindwa kukabiliana na changamoto zinayoyabaliki licha ya kwamba Mataifa hayo yanategemea Kilimo kwa asilimia zaidi ya 70%.
“ Florida University iwe kiungo cha kuunganisha Taaluma katika vyuo vikuu vya nchi changa kikiwemo kile cha suza ”. Alisema Balozi Seif.
Mapema Rais wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida
{ famu } Dr.James Ammons alisema Chuo hicho kinalenga kujenga nguvu ya Taaluma katika kuona kizazi cha sasa kinapata Elimu inayokwenda sambamba na mabadiliko ya kasi ya Sayansi na Teknolojia Duniani.
Dr. ammons alisema Chuo hicho kilichoanzishwa miaka 125 iliyopita kimefungua masomo ya Taaluma ya Madawa na Sheria yakianguliwa nay ale ya Kilimo na Ufundi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata fursa ya kukitembelea kitengo cha Ufundi cha Chuo hicho cha Florida
{ FAMU -FSU }.
Mkuu wa Kitengom hicho cha ufundi Dr. Regional Perry alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake hatua waliyofikia chuoni hapo ya kifanya utafiti katika masuala ya Madawa na Wanaadamu.
Dr. Perry alisema wataalamu wa chuo hicho tayari wamefikia hatua ya kutengeneza Injini za vyombo vya moto.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment