Monday, August 22, 2011

Waasi waiteka Tripoli

Maelfu ya wakazi wa Tripoli wamekuwa wakisherehekea usiku kucha wakati wapiganaji walipoingia katika uwanja mashuhuri ambao wameubadilisha jina lake mara moja na kuitwa uwanja wa mashujaa ambako wa Libya waliokuwa na furaha walianza kuangusha na kuharibu mabango makubwa ya picha ya bwana Gadhafi na kuanza kuyakanyaga.
Hadi hivi karibuni serikali ya Libya imekuwa ikiutumia uwanja huo kuanda maandamano makubwa ya wananchi kuonesha uungaji mkono wa kiongozi wa Libya ambaye anaonekana kuwa ameshindwa hivi sasa.
Viongozi wa upinzani hata hivyo wamekiri alfajiri ya Jumatatu kwamba kungali kuna maeneo ambayo kuna upinzani ndani na nje ya Tripoli. Msemaji wa upinzani amesema wapiganaji wameshauzingira uwanja wa Bab Alazizya ambako wanaamini huwenda bwana Gadhafi amejificha lakini wanasita kuanza kushambulia.
Msemaji wa waasi anasema walipeleka kundi la wapiganaji kuingia katika mji mkuu kupitia bahari kutokea bandari ya Misrata. Aliongeza kusema kwamba kikosi maalum cha ulinzi wa Gadhafi kimejisalimisha na hivyo kuwawezesha wapiganaji kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya mji

No comments:

Post a Comment