Thursday, August 25, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HIZB UT- TAHRIR AFRIKA MASHARIKI YAWASILISHA ‘SHUTUMA YA DHULMA DHIDI YA WAISLAMU’ KWA UBALOZI WA PAKISTAN
Tarehe 12/08/2011 Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki iliwasilisha rasmi shutma kwa ubalozi wa Pakistan jijini Dar-es-Salaam dhidi ya vitendo vya nchi hiyo vya dhulma, maonevu na unyakuzi wa kuwatia nguvuni kisiri wanaharakati wa Kiislamu wasio na hatia, kwa ‘kosa’ tu la kuulingania Uislamu kifikra bila ya kujihusisha na kitendo chochote cha nguvu.
Shutuma hizo ziliwasilishwa na Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki (Masoud Msellem) na Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano ya Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki (Sheikh Mussa Kileo), na kukabidhiwa Afisa Utawala na Mwambata wa ubalozi wa Pakistan nchini Tanzania bwana Masud Hassan Khan. Pamoja na shutma hizo Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki iliwasilisha pia waraka maalum uliotolewa na Hizb ut-Tahrir ndani ya Pakistan, unaotaja kinaga ubaga majina na mazingira ya unyakuzi wa Naibu msemaji wa Hizb ut-Tahrir Pakistan (Imran Yousafzai) na wanachama wengine waandamizi wa Hizb ut-Tahrir ndani ya Pakistan akiwemo Hayan Khan, Ousama Hanif na Dk. Abdul-Qayuum. Wote walinyakuliwa kisiri na wanaendelea kushikiliwa mafichoni pa siri kwa dhulma na serikali ya Pakistan bila ya hatia yoyote. Aidha Hizb ut-Tahrir Afrika ya Mashariki iliisisitiza (demand) serikali ya nchi hiyo kuwacha vitendo hivyo vya dhulma mara moja na kuwaachia huru Waislamu hao. Shutuma kama hizi pia ziliwasilishwa kwa ubalozi wa Pakistan jijini Nairobi kwa kupitia Mwakilishi wa Vyombo vya Habari wa Hizb ut-Tahrir Afrika ya Mashariki (Shabani Mwalimu)
Licha ya Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki kulaani kwa nguvu zote dhulma na uonevu huu na kuwataka Waislamu wote na kila mwenye chembe ya ubinaadamu kulaani unyama huu na kufanya upeo wa jitihada ili wahanga waachiwe huru. Pia tunatangaza kwa sauti ya juu kwamba dhulma na mateso hayawezi kamwe kuzuia Hizb kuendelea na kazi yake tukufu ya kulingania Uislamu kama mfumo bora mbadala hadi hatima ya kuasisi serikali yake, Khilafah Rashidah katika nchi kubwa za kiislamu kama ilivyobashiriwa na Allah Ta’ala na Mtume Wake (SAAW), ili kuukomboa ulimwengu mzima na uovu wa mfumo wa kibepari ukiwemo kukamata na kutesa watu kwa kutangaza haki. Siku hiyo, madhalimu watajuta lakini majuto yao hayatuwasaidia chochote!
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment