Thursday, August 18, 2011

kutatua migogoro kwa njia ya amani

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishauri jamii kuendeleza utamaduni ya kutatua migogoro inayowazunguuka kwa njia na majadiliano ili kuepuka unyakuzi wa haki na maisha ya wananchi. Amesema majadiliano yanaondoa matumizi mabaya ya silala, uhasama na hatimaye kuepusha shari inayoweza kuzaa maafa.
Balozi Seif amesema hayo baada ya kuangalia eneo huru la kiuchumi lililoleta mgogoro baina ya vijiji vya wingi na maziwang'ombe micheweni Pemba na kupelekea Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni Kuunda tume ya kusuluhisha mgogoro huo kwa njia ya majadiliano. Akizungumza na Viongozi wa Tume hiyo hapo Skuli ya Micheweni Balozi Seif amesema uwamuzi wa pamoja wa majadiliano kati ya pande hizo mbili umeleta faraja kwa Serikali na kupelekea wananchi wa eneo hilo kuishi kwa raha na amani.
Ameupongeza uwamuzi huo ambao hata Jumuiya ya Kimataifa zinautumia katika kutafuta suluhu za matatizo mbali mbali yanayotokea baina ya jamii au mataifa tofauti. ''Tungeendelea na vurugu za kukaribisha kutumika kwa marungu na mapanga tusingefikia hatua hii iliyoleta faraja kwetu sisi hasa viongozi wa ngazi za juu wa serikali'' Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Amewapongeza wananchi wa Wingwi na Maziwa ngo'mbe kufikia hatua hii ya amani na kuvishauri vijiji vyengine kuiga mfano huu. Amesema bado ipo migogoro kama hii kwa baadhi ya vijiji hapa nchini na cha kuzingatia ni kuona hatua ya mafakiano inafikiwa kwa kutumia tume za majadiliano baina ya pande zinazohusika na mgogoro.Mapema Mkuu Wilaya ya Micheweni nd. Juma Abdulla amesema eneo hilo la maeneo huru ya serikali ambalo lieasisiwa tokea mwaka 1992 linawapa fursa wananchi wa maeneo hayo kulitumia kwa vipando vidogo vidogo vya muda hadi hapo serikali kuu itapokuwa tayari kuwekeza. Nd. Juma amesema tamaa ya baadhi ya watu kuhodhi ardhi bila ya kuzingatia taratibu zilizopo ndio inayopelekea kuleta migogoro ya ardhi

No comments:

Post a Comment