Sunday, August 21, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitosita kuwachukuliwa hatua za kisheria muda si mrefu viongozi wote waliohusika na masuala ya uvushaji wa magendo ya zao la karafuu nje ya Nchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Mabalozi wa CCM wa Mashina yaliyomo ndani ya Wadi ya Fujoni hapo Afisi ya CCM Tawi la Fujoni Wilaya ya Kaskazini B.
Balozi Seif amesema Viongozi waliohusika na Biashara hiyo ya Magendo ya Karafuu wanajuilikana na hatua ya kuwachukula sheria ina lengo la Kulinda Heshima ya Serikali. Amesema uamuzi wa Serikali wa kupandisha bei ni kuimarisha pamoja na kushajiisha uzalishaji wa zao hilo ambalo ni uchumi na muhimili wa Uchumi wa Taifa. “Hakuna sababu tena ya zao la Karafuu kuuzwa nje ya Nchi Kimagendo kwa vile bei ya bidhaa hiyo imepandishwa kuzingatia soko la Dunia ” . Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Amewaomba wakulima kuzidi kuimarisha kwa wingi uzalishaji wa mikarafuu mipya kwa lengo la kujiongezea kipato chao na kupunguza makali ya maisha. Akizungumzia suala la uchaguzi wa Viongozi wa CCM utakaofanyika Hapo mwakani Balozi Seif ambae pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM amewatahadharisha Mabalozi hao kuwa makini katika kuepuka tabia ya kutanguliza ujomba katika kuchagua Viongozi.
Balozi Seif amesema ni vyema ikaeleweka kwamba wanayemchagua anafaa kuwaongoza akiwa na vigezo vyote vya uongozi. Amesisitiza kwamba Tabia ya kuendeleza urafiki katika suala la uongozi inapunguza sana nguvu za chama. Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kitope amemaliza ziara yake ya kukutana na Mbalozi wa Mashina ndani ya Jimbo hili
Othman khamis ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment