Wednesday, September 21, 2011

PRESS RELEASE

Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya migodi Afrika { AFRICA BARICK GOLD } inakusudia kuandaa ampango wa kusaidia vifaa vya uokozi kwa vyombo vya usafiri wa baharini kwa lengo la kupunguza maafa wakati zinapotokea ajali baharini.
Mjumbe wa Bodi hiyo Balozi Bakari Mwapachu ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha salamu za rambi rambi kwa mweyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Balozi bakari Mwapachu amesema utafiti unaonyesha kwamba vyombo vingi vya usafiri wa baharini haviwezi kutosheleza vifaa vya uokozi wakati vinapopatwa na ajali.
Amesem Uongozi wa Bodi hiyo utaandaa utaratibu wa kuzungumza na Taasisi na Mamlaka zinazosimamia usafiri wa baharini ili kuona mpango huo unaanza kutekelezwa ambapo utahusisha pia na vyombo vidogo vidogo vya uvuvi.
Balozi Mwapachu ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga Hoja kwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Afrika Mashariki kwa kuishauri iangalie mazingira ya kujenga kituo cha Mawasiliano Hapa Zanzibar. Bodi hiyo imetowa mkono wa pole kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia shilingi Milioni 60,000,000/-,
Taasisi nyengine zilizochangia mfuko wa maafa ni kampuni ya Elewana Afrika inayoendesha Biashara ya Hoteli Tanzania pamoja na Uongozi wa chama cha NCCR Mageuzi .
Mweyekiti wa Chama hicho Bwana James Fransis Mbatia amesema changamoto iliyopo ni watu wote wenye mapenzi na janga hili wanaongeza ushirikiano katika kusaidia kukamilisha kutatua tatizo hili.
Akipokea michango hiyo Mwenyekiti Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif ameendelea kuzisukuru Taasisi na jumuiya zilizojitolea kusaidia tatizo hili la maafa ya kuzama kwa meli Zanzibar.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment