Wednesday, September 21, 2011

Muktasari wa Sensei Rumadha Fundi ”Romi”(Sandan)Rumadha Fundi, “Sensei Romi”Mvuto wangu katika sanaa ya Karate ulianza wakati nilikuwa mdogo mnamo miaka '70s pale Kariakoo,jiji Dar, lakini asili ya kwetu ni Tabora. Kwa bahati nzuri, jirani yetu pale mtaani(Aggrey/Congo) Dar-es-salaam ambako Sensei Bomani alikuwa anakuja kuwafuata baadhi ya wanafunzi wake enzi hizo. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kujua hasa kuhusu Goju Ryu Karate.
Mwaka '78 mwishoni nilipata fursa ya kutembelea “Hekalu la Kujilinda” Zanaki Dojo Kan Shibu, nakuongea na Senpai Magoma Nyamuko Sarya. Kipindi hicho Sensei Bomani alikuwa amekuja toka Marekani na kuja kuwafanyia mitihani wa daraja la “Nidan”kina Senpai Magoma Nyamuko Sarya (Mwafunzi kiongozi), Senpai Tola Sodoinde Malunga, Sensei Gamanya nk. Ndipo nilipoanza shughuli za mafunzo kama”Teenager class”lilijulikana kama (Bomani Brigade)
Baada ya mtiani wa mkanda wa kahawia '81, kiongozi wetu (Senpai Magoma) aliondoka kwenda India na Phillippines kusomea sanaa mbalimbali na Yoga , ndipo na mimi nikajiunga nae huko India na baadae kwenda Sweden mnamo mwaka wa '85 katika shule ya Yoga”Internation school of Intution Practice” au katika lugha ya Sanskrit ambayo ndio inatumiwa na Yoga hujulikana kama “Prakshimata - Ananda Nilayam” huko, Gullringen, Vimmerby, Sweden.
Hapo ndipo lipohitimu ualimu wa Yoga baada ya kozi ya miaka miwili na kurudi tena Calcutta, India kwa Master mkuu wa Yoga duniani na hatimae kupata ngazi ya juu katika mafunzo ya Yoga mnamo mwaka wa '90 “Avadhuta”.
Vile vile nilipata fursa ya kwenda Houston, Texas mwaka '88 na kuendelea na mafunzo ya Karate mtindo wa “Okinawa Goju Ryu” chini ya uongozi wa Master Sensei Morio Higaona mwenye Dan 10, kiongozi mkuu wa “International Okinawan Goju Ryu Karate -Do Federation” na kupata fursa ya kupata daraja la kwanza '89 toka kwa Master Higaona huko Tampico, Mexico chini ya uongozi wa Sensei Mario Falcone wa Mexico na Sensei Ramon Veras wa Houston, Texas. Hawa ni moja ya walimu walio nisaidia kwa dhati katika sanaa ya Karate. Ninapenda kutowa shukran nyingi kwa walimu wote ambao waliweza kunifundisha sanaa hii sehemu zote zile nilizoweza kushiriki katika fani hii kama vile, Master Morio Higaona, Master Teruo Chinen, Sensei kiongozi wa Okinawa Goju Ryu, in Okinawa, Sensei Matsuda, na Sensei Muramatsu.Hao wote ni viongozi wa ngazi za juu sana duania katika sanaa ya mtindo wa Goju.
Kwa sasa hivi nina daraja la tatu “Sandan”mkanda mweusi kwa muda mrefu sasa. Kumbu kumbu yangu kubwa ni kuwa na ushirikiano mwema na wanafunzi wengi wa zamani pale “Hekalu la Kujilinda” ambao sasa hivi bado wapo mbele katika kusaidia vijana kama Sensei Maulid Pambwe, Rashid Almas, Mohamed Murudker, Wilfred Melkia, Geofrey Sawayael “Shoo”, Mbezi, Metthew huko Mwanza, Ndaukile,Edgar Kaliboti huko Sidney Australia, Salum Kitwana Khamisi huko UK. Hata wale wote ambao nimewasahau popote pale duniani.
Pia, natoa shukran nyingi sana kwa mtu muhimu sana katika maisha yangu ya kisaa ya Karate na Yoga ambaye ulikuwa ndio mashine ya mafanikio yangu ngazi zote hizo, Senpai Magoma Nyamuko Sarya(Mahadev/Mrnal) popote pale alipo nasema,”Shkran”.
Mipango ya uendelezaji sanaa hii kwa miaka ya mbele huko Tanzania ni muhimu sana. Moja ya hiyo mipango ni siku moja kufungua chuo cha sanaa ya kujilinda na kutumia nyezo za Karate”Kobudo” Kama vile “Sai, Tonfa, Nunchaku,Bo, Shuri, “Three section Nunchaku” nk. Kwa ajili ya kufundisha Tanzania. Ingawa sio leo wala kesho, bali ni moja ya mipango ya mbele huko katika maisha nitaporudi Tanzania, nakuwashirikisha walimu wengine wenye uzoefu mwingi katika kutumia nyenzo hizo.

No comments:

Post a Comment