Monday, November 28, 2011

Kombe la Mapinduzi Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Mpango wa kuandaa Kombe la Mapinduzi Cup umelenga kukuza Michezo pamoja na kuimarisha Ujirani mwema ndani ya Mipaka ya Afrika Mashariki.
Balozi Seif ametoa kauli hiyo wakati akizindua Kamati ya Mapinduzi Cup yenye wajumbe kumi ikiongozwa na mwenyekiti wake Mohd Raza Hassan katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Alisema mpango huu unaweza kuongeza kiwango cha Michezo ndani ya kanda hii endapo Wapenda michezo na wadau wote wataonyesha ushirikiano wao kwa kamati hii.
Balozi Seif alisisitiza kwamba Serikali haina budi kuiunga mkono Kamati hii ili kuona inafanikisha malengo iliyopangiwa.
“ Na hili nitahakikisha litatekelezwa kwa upande wa Serikali Mimi mwenyewe nitalisimamia kwa vile ndie Mtendaji Mkuu wa Serikali ”.
Alisisitiza Balozi Seif.
Aliipongeza Kamati hii kwa kuwa na wajumbe mahiri na ana matumaini ya kufanikiwa na Kamati hiyo na kuvuka kiwango cha ufanisi cha mwaka uliopita.
Akimkaribisha Balozi Seif Waziri wa Hahabi ,utamaduni, Utalii na Michezo Abdillahi Jihadi Hassan amesema Wizara ina matuimaini makubwa na Kamati hiyo kwa vile imeundwa kwa kuzingatia uwezo na uzoefu walionao.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup Mohd Raza ameahidi kwamba Kamati yake itahakikisha inatekeleza vyema majukumu yake kwa mujibu wa matakwa ya wadau wa Michezo.
Raza alisema Kamati yao itaendelea kuzingatia zaidi huduma na burdani kwa wananchi katika mashindano ya michezo ya Mapinduzi Cup yatakayojumisha Pia Mpira wa Wavu { Netball } kwa kuzhishirikisha baadhi ya Timu za Tanzania na timu alikwa kutoka nje ya Afrika Mashariki.
Kamati hiyo iliyoundwa chini ya uwenyekiti wa Mohd Raza ina wajumbe kumi ambao ni Sherry Khamis, Ibrahim Makungu, Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Jazira, Katibu Mkuu Wizara ya Habari utamaduni na Mchezo Ali Mwinyikai na Naibu wake Issa Mlingoti.
Wengine ni Ali Khalil Mirza, Taufiq Turky, Aboubakar Bagharesa pamoja na Farouk Karim ambaye ndie Mratibu wa Kamati hiyo.
Othman Khmis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Elimu ya juu Zanzibar

Taasisi za Elimu ya Juu Nchini zina wajibu wa kuhakikisha idadi ya wanafunzi wa Kike kuingia Vyuo Vikuu inaongezeka ili kukidhi mahitaji ya Jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo kwenye mahafali ya tano ya Chuo Kikuu cha Arusha ambapo jumla ya wahitimu 600 wamemaliza masomo yao ya shahada ya kwanza na Diploma katika Fani za Biashara, elimu na Ustawi wa Jamii.
Balozi Seif alisema ongezeko hilo litaondosha kabisa pengo kubwa liliopo kati ya Wanafunzi wa Kike na Kiume katika Elimu ya Vyuo Vikuu hapa Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuagiza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Arusha kuongeza Mikakati madhubuti ili kuleta uwiano wa Wananfunzi wa Jinsia zote.
“ Tafiti zinaonyesha kwamba kumuelimisha Mwanamke sawa na kuwaelimisha watu kumi. Hii inamana kwamba familia itaelimika haraka iwapo kutakuwa na mmoja wa Mwanamke aliyepata elimu” Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi.
Alifahamisha kwamba vyuo Vikuu Vikuu lazima vishirikiane na Serikali katika kuona Dira ya Taifa ya Maendeleo ishirini ishiri
{ Vission 2020 } inafikia malengo yake.
Balozi Seif aliitaja changamoto inayowakabili wana vyuo Vikuu ni namna gain wanaweza kutumia Taaluma yao kushajiisha Sekta Binafsi katika kuibua ajira ndani ya Jamii.
Alisema hatua hiyo itakwenda sambamba na mipango ya Serikali zote mbili za kuandaa mazingira bora ya kuongeza fursa katika soko la ajira hasa kwa kundi kubwa la Vijana.
Katika risala yao iliyotolewa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuoni hapo Nd. Joshua Onyango wameiomba Serikali kuwapunguzia matatizo yanayowakabili ya Ubovu wa Bara bara, Huduma za Maji safi pamoja na Huduma za Umeme.
Wamesema matatizo hayo kwa kiasi kikubwa yanachangia kupunguza ari yao ya kujipatia Taaluma kwa utulivu ambayo ndio lengo la kuwepo kwao Chuoni hapo.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Arusha Dr. Laban Mgedi alisema lengo la chuo hicho ni kuongeza asilimia 32% ya wanafunzi wa kike Chuoni hapo.
Dr. Laban amefahamisha kwamba Afrika inahitaji wasomo wa fani tofauti wakiwemo wanawake ili kuleta Mapinduzi ya haraka ya Elimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Mahfali hayo pia aliweka jiwe la Msingi la Jengo la Michezo la Chuo hicho.
Jengo hilo linalotarajiwa kukamilika ujenzi wake mwezi Febuari mwakani linatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania Milioni mia mbili.
Kukamilika kwa jengo hilo kutatoa afuaeni kwa wanafunzi kuwa na darasa la uhakika la masuala ya Sanaa na Utamaduni chuoni hapo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Saturday, November 26, 2011

Tubadilike kokomesha ajira za watoto

Inaonekana bado jamii haijataka kubadili tabia ya kukomesha ajira mbaya kwa watoto kama ambvyo mtoto alivyokutwa akifanya biashara za kitalii pembezoni mwa fukwe za bahari ya Bagamoyo, hii ni ajira mbaya zaidi kwani kwa asilimia mia moja mtoto huingia kwenye matatizo ya unyanyasaji wakijinsia n.k

Thursday, November 24, 2011

Bara la Afrika limefanikiwa katika kupunguza migogoro kwa kutumia mbunu mwafaka

Changamoto kubwa inayolikabili Bara la Afrika Hivi sasa katika kuelekea kwenye Maendeleo zaidi ni kutumia mbinu na Marifa yaliyopelekea kupunguza migogoro ya Kijamii katika baadhi ya Mataifa ndani ya Bara hili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Viongozi na Wataalamu wanaoshughulikia Kuondosha migogoro Barani Afrika unaofanyika huko katika Hoteli ya Melia iliyopo Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif alisema Jamii ya Kimataifa imeshuhudia utatuzi wa Migogoro kadhaa Barani Afrika hali ambayo kwa kiasi kikubwa imepunguza Migogoro na hata Mauaji ya Raia wasio na hatia. Aliwataka Viongozi na Wataalamu hao kutumia fursa nzuri iliyopo ya Amani iliyorejea Barani humu kwa kuweka Mipango bora itakayoleta faraja zaidi ya ustawi wa Jamii katika miaka ijayo.
“ Tumeshuhudia utulivu wa Kisiasa ilivyorejea ndani ya Bara hili hasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu eneo ambalo Sudan na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo { DRC } zilikuwa katika migogoro mikubwa ya Kisiasa ”. Alikumbusha Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea matumaini yake kwamba Ripoti itakayotolewa na Viongozi hao baada ya kumalizika Mkutano wao itawezesha kujenga mazingira bora ya kudumisha Amani Barani Afrika.
Balozi Seif amezipongeza Taasisi zilizoandaa Mkutano huo ile ya Mwalimu Nyerere, Kituo cha Hali za Binaadamu cha Kimataifa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Norway kwa uamuzi wao wa kufanya Mkutano huo Hapa Zanzibar na hasa ndani ya Jimbo lake ya Kitope.
Alisema uwamuzi wao huo haukuwa wa kubahatisha bali imekuja kwa kuzingatia sifa ya Zanzibar ya amani iliyopelekea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa { GNU } kufuatia Mgogoro wa muda mrefu uliovihusisha Vyama vya CCM na CUF.
Balozi Seif aliwaeleza Washiriki wa Mkutano huo kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inafanya kazi zake vyema huku ikikabiliwa na changa moto kubwa ya kutekeleza matarajio ya Wananchi wote wa Zanzibar.
Akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim alisema yapo Maendeleo makubwa ya kupunguka kwa Migogoro Barani Afrika jambo ambalo limeleta faraja kwao akiitolea mfano nchi ya Sudan.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Haki za Binaadamu bwana David Harland ameipongeza Zanzibar kwa ukarimu wake unaopelekea kupokea Vikao na Mikutano Mzizito ya Kimataifa ndani na nje ya Bara la Afrika.
Wakati wa Mchana akiwa Mkoani Dodoma Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana wa Uongozi wa Kampuni ya uwekezaji vitega uchumi inayojishughulisha na Mradi wa umeme unaotumia upepo na jua kutoka Nchini India.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni hiyo ya Indomount bwana sudhakar amesema Taasisi yake imepanga kutumia Jumla ya Dola za Kimarekani Bilioni Moja kati ya Bilioni saba zilizotengwa na waziri mkuu wa Nchi hiyo kusaidia Serikali na Taasisi Binafsi Barani Afrika.
Naye Balozi Seif ameuomba Uongozi wa Kampuni hiyo kuangali Meneo ambalo wanaweza kusaidia kati ya yale yaliyoainishwa na kupendekezwa na Zanzibar katika mipango yake ya Maendeleo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Tuesday, November 22, 2011

Uongozi mpya wa Singida Press Club

Safu ya waliosimama nyuma ni Emmanuel Michael (Katibu Msaidizi), Abby Nkungu (Katibu Mtendaji), Seif Takaza (Mwenyekiti) na Rev Immanuel Barnaba (Mjumbe).
Walio simama safu ya mbele ni Nathaniel Limu (Mweka hazina Msaidizi), Joseph Lujuo (Mjumbe), Awilla Silla (Mweka Hazina)na Elisante John (Mjumbe).

Sunday, November 20, 2011

New leaders of Singida Press Club

THE Annual General Meeting of the Singida Press Club (SINGPRESS), has elected Seif Takaza, as a new Chairman for three years term with effect from November 18, this year.
Takaza has taken over from Rev Immanuel Barnaba who did not defend his title but opted for another post. Prior to the elections, Takaza was the Assistant Executive Secretary.
It was not an easy task for Takaza to acquire the prestigious post. A re-run voting had to be conducted after another candidate who was eyeing the same post, Damiano Mkumbo, tied points with him.
Abby Nkungu bounced back to leadership in style after staying on the sidelines watching for three years following his resignation in 2008. He was elected the Club’s Executive Secretary pushing aside miserably the incumbent Doris Meghji.
Awila Silla, the only lady in the SINGPRESS new lineup, was elected treasurer. Jumbe Ismael was elected Vice Chairman, Emmanuel Michael picked the Assistant Secretary and Nathaniel Limu , the clubs assistant treasurer.
Rev Immanuel Barnaba, Elisante John and Joseph Lujuo were elected members of the executive committee.
The AGM also fired from being SINGPRESS member, Hillary Shoo, after he was found guilty of gross misconduct and behaving contrary to journalistic code of ethics.
Opening the meeting, Singida Regional Commissioner Dr Parseko Kone called on all scribes in the region to uphold their professional ethics saying that would enable the community surrounding them hold the profession in high esteem.
He further asked the journals to be impartial and stick to professionalism by giving fair coverage to all and sundry without fear or favor.
The elections were presided over by the Singida Regional Social Welfare Officer, Zuhura Karya and witnessed by Assistant Programme Officer from Union of Tanzania Press Clubs (UTPC, Victor Maleko

New leaders of Singida Press Club

THE Annual General Meeting of the Singida Press Club (SINGPRESS), has elected Seif Takaza, as a new Chairman for three years term with effect from November 18, this year.
Takaza has taken over from Rev Immanuel Barnaba who did not defend his title but opted for another post. Prior to the elections, Takaza was the Assistant Executive Secretary.
It was not an easy task for Takaza to acquire the prestigious post. A re-run voting had to be conducted after another candidate who was eyeing the same post, Damiano Mkumbo, tied points with him.
Abby Nkungu bounced back to leadership in style after staying on the sidelines watching for three years following his resignation in 2008. He was elected the Club’s Executive Secretary pushing aside miserably the incumbent Doris Meghji.
Awila Silla, the only lady in the SINGPRESS new lineup, was elected treasurer. Jumbe Ismael was elected Vice Chairman, Emmanuel Michael picked the Assistant Secretary and Nathaniel Limu , the clubs assistant treasurer.
Rev Immanuel Barnaba, Elisante John and Joseph Lujuo were elected members of the executive committee.
The AGM also fired from being SINGPRESS member, Hillary Shoo, after he was found guilty of gross misconduct and behaving contrary to journalistic code of ethics.
Opening the meeting, Singida Regional Commissioner Dr Parseko Kone called on all scribes in the region to uphold their professional ethics saying that would enable the community surrounding them hold the profession in high esteem.
He further asked the journals to be impartial and stick to professionalism by giving fair coverage to all and sundry without fear or favor.
The elections were presided over by the Singida Regional Social Welfare Officer, Zuhura Karya and witnessed by Assistant Programme Officer from Union of Tanzania Press Clubs (UTPC, Victor Maleko

Volunter wa UTPC

Mwandishi wa habari kutoka Ujerumani Jenis Westphal ambaye yupo kwenye afisi za UTPC akifanya kazi za kujitolea kama mwandishi wa habari na mpiga picha kwenye afisi za UTPC zilizopo jijini Mwanza
Jenis Westphal akiwa afisini za UTPC Mwanza

Saturday, November 19, 2011

Friday, November 18, 2011

Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Sauti za Busara

Sauti za Busara Zanzibar yahitaji wafadhali wengi zaidi ili kuhakisha kwamba tamasha hili linaweza kuendelea zaidi na hasa katika kuimarisha Utamaduni wa Zanzibar pamoja na kukusa soko la Utaii visiwani Zanzibar

Thursday, November 17, 2011

mkutano wa Waandishi na Wadau wa Habari uliofanyika tarehe 08.10.2011, katika ukumbi waEACROTANAL Zanzibar, Mkutano huo uliandali na ZPC na UTPC

Waandishi wakiwa katika mkutano wa pamoja na wadau wa habari, mkutano ambao ulifanyika kawenye ukukmbu wa Eacrotanal Zanzibar

Katibu Mtendaji na Naibu Katibu wa ZPC wakiwa kwenye Mkutano wa wadau na waandishi wa habari
Waandishi na wahariri wa habari kutoka kwenye vombo mabali mbali wakifuatilia kwa makini mada ya Utawala bora kwenye vyombo vya habari kwenye mkutano uliowakutanisha waandishi na wadawa wa habari nchini

Waandishi na Wadau wahabari wakiwa wamesima pamoja katika kuwaombea dua ndugu na jamaa waliofariki kwenye ajali ya meli ya Mv Spice Islanders hivi karibu visiwani Zanzibar



Mkurugenzi wa Shirika la Utaangazaji la Zanzibar mwenye kipaza sauti akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki katika mkutano kati ya waandishi na wadau wahabari

Mjumbe kutoka kwenye jumuiya ya Zanzibar Youth Forum akichangia mada

Mtangazaji kutoka Chuchu Fm akichangia mada

Mtangazaji kutoka Bomba Fm akichangi mada

Katibu Mkuu wa PPC akichangia mada kwenye Mkutano wa wadau na waandishi wa habari



Mjumbe kutoka AIDNET Zanzibar akichangia mada

Mwakilishi kutoka katika Idara ya Ustawi wa Jamii akichangia mada


Mjumbe kutoka chama cha AFP akichangia madaMwandishi wa The Gurdian akichangia mada


Mwasilishaji mada, ambaye pia ni mshauri katika masuala ya habari

Mwenyekiti wa ZPC akifungua mkutano wa Wadau na Waandishi wa Habari, mkutano ambao uliendesha na kusimamiwa na ZPC na UTPC.Picha zote ma Haroub Hussein Khamis wa Zanzibar Press Club

Monday, November 14, 2011

Balozi Seif akiwa na wageni waliomtembelea afisini kwake




MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKISALIMIANA NA MJUMBE WA KAMATI YA SIASA NA KAMATI KUU YA CHAMA CHA KIKOMINISTI CHA CHINA CCP BW, LIU YUNSHAN ANAEONGOZA UJUMBE WA WATU 21 WALIOFIKA OFISINI KWA BALOZI SEIF ILIOPO MTAA WA VUGA MJINI ZANZIBAR BW LIU YUNSHAN AKISISITIZA JAMBO WAKATI WA MKUTANO WAKE NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI KATIKA MKUTANO HUO BALOZI SEIF AMESEMA KUWA JAMHURI YA WATU WA CHINA ITAENDELEA KUWA KIUNGO MUHIMU KATIKA HARAKATI ZA KUSAIDIA UCHUMI NA MAENDELEO YA TANZANIA
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKISALIMIANA NA KATIBU MKUU WA MIKUTANO YA KIMATAIFA YA UKANDA WA MAZIWA MAKUU BALOZI LIBERETE MULAMULA ALIYEIKA OFISINI KWAKE VUGA MJINI ZANZIBAR


Sunday, November 6, 2011

100% yafunika Nungwi

Sherehe za maridhiano na umoja wa kitaifa zilizoandaliwa na taasisi ya Swahili Center zinaendelea kwa kasi ambapo kwa Ijumaa iliyopita, vikundi vya Nyota ya Umoja (Maigizo,Nungwi) na Mkota Ngoma (Mkoani, Pemba) vilirindima katika kijiji cha Nungwi, Unguja.
Katika onesho hilo ambalo lilifanyika katika Uwanja wa Skuli ya Nungwi, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wapenzi wa fani za sanaa za maonesho kutoka sehemu mbali mabli waliliminika na kujimwaga katika burudani hizo zilizoanza saa 10 alasiri.
Kundi la Maigizo la Nyota ya Umoja, maarufu kwa michezo yao kama vile ‘Dhulma Kafara’ na ‘Masikini naye Mtu’, walitoa burudani safi kupitia mchezo wa ‘Mchelea Mwana Kulia’ uliobeba maudhui ya umuhimu wa ushirikiano wa kuyalinda maadili ya KiZanzibari ndani ya jamii.
Nalo kundi la Mkota Ngoma kutoka Mkoani, walikonga nyoyo za wapenzi wa Ngoma na asili kwa kupiga ngoma zao za Msembwe, Unjunguu na Kumbwaya. Wengi waliohudhiria shehere hizo walivutiwa sana na umahiri wa kundi hilo katika kuzicheza Ngoma hizo.
Katika kuutambulisha mradi huo kwa waliohudhuria onesho hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Swahili Center Bw. Kheri Abdalla Yussuf, aliwajulisha wapenzi hao wa sanaa za utamaduni kuwa dhamira ya mradi huo ni kuimarisha misingi ya umoja wa kitaifa nchini Zanzibar kupitia sanaa za utamaduni zenye burudani na mafunzo kwa jamii yote.
Wakati huo huo, aliyekuwa mgeni rasmi katika onesho hilo, Mhe. Bi Riziki Juma Simai (Mkuu wa Wilaya ya Kasakazi A) aliwataka wananchi wa Nungwi na wote waliohudhuria kuimarisha misingi ya umoja wa kitaifa kwa vitendo.
Mradi wa 100% Zanzibari (tafsiri; Mzanzibari asilimia mia moja) umekuwa ukifanya maonesho katika Mikoa ya Unguja na Pemba kufuatia kambi za kisanii zinazoshirikisha fani za Taarab, Ngoma za Utamaduni na michezo ya Kuigiza. Shangwe hizo zimekuwa zikifanyika kwa awamu katika sehemu mbali mbali ambapo kwa kipindi cha Nov 15-19 zitahamia katika Mkoa wa Mjini Maghribi.
Swahili Performing Arts Center (Kituo cha Sanaa za Maonesho cha Waswahili) ni taasisi ya iliyoanzishwa kwa dhamira ya kuchangia katika maendeleo ya sanaa za maonesho asilia za Zanzibar pamoja na zile za mwambao wa Waswahili kupitia uwezeshaji (wasanii), uzalishaji wa kazi za sanaa, maonesho na ushirikishaji jamii. Dira ya Swahili Center ni kuurejeshea hadhi utambulisho wa utamaduni wa Kiswahili.
Mradi wa 100% Zanzibari umedhaminiwa na Ubalozi wa Norway pamoja na kampuni ya mawasiliano ya Zantel.
Kheiri A.Y. Jumbe
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji

Robert Shumake akubali ombi la Balozi Seif Ali Iddi

Mamlaka ya Mitaji na Mendeleo ya Jamii ya wa Michigan Nchini Marekani imekubali kuisaidia Zanzibar katika masuala ya Elimu, Afya na Mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bwana Robert Shumake ametoa kauli hiyo wakati wa mazungumao yake na makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mwishoni mwa ziara yake Nchini Marekani.
Bw. Shumake ambaye tayari ameshakutana na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ ambao umenambatana na Balozi Seif katika ziata hiyo mamlaka hiyo inajitayarisha kuongeza misaada yake kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar.
“ Tumeshatoa misaada ya vifaa vya elimu kwa Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Ethiopia na Tanzania katika skuli za Mkoa wa Kilimanjaro” Alisema Bwana Shumake.
Alisisitiza kuwa Mamlaka yake imekuwa ikitoa fursa za kudhamini masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa Afrika wenye mazingira magumu.
Bwana Shumake alisema utafiti uliofanywa na Mamlaka yake umegundua watoto wengi wa Bara la afrika wanashindwa kuendelea na Masomo ya juu kutokana na kukabilkiwa na umaskini uliokithiri.
Alimueleza Balozi Seif kwamba bado wanaangalia uwezekano wa kutoa huduma katika sekta za Kilimo ikilenga zaidi vijana ambao kundi kubwa linakosa ajira na kujikimu kimaisha.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ameipongeza Mamlaka hiyo kwa uwamuzi wake wa kusaidia huduma za kijamii.
Balozi Seif alisema Familia nyingi hasa za kiafrika zimekuwa zinakosa huduma za kijamii na kukumbwa na maradhi. Balozi Seif na Ujumbe wake unaondoka Marekani na unatarajiwa kuwasili nchini jioni ya Jumatatu ya tarehe 8/11/2011.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziba

Zanzibar yashauriwa kuwatumia vyema waatalamu wake

Zanzibar imeshauriwa kuangalia njia za kuwatumia vyema Wataalamu Wazawa walioko nje ya Nchi ili kuharakisha kasi ya Maendeleo ya Jamii .
Ushauri huo umetolewa na Kiongozi wa Wazanzibari waliopo Nchini Marekani ambao wako katika hatua za mwisho kuandaa Jumuiya itakayoitwa Zanzibar Diascora Organization Dr. Omar Haji Ali wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozo Seif Ali Iddi kwenye Hoteli ya Crown Plaza Mjini Washington DC. Nchini marekani.
Dr. Omara alimueleza Balozi Seif kwamba lengo la Jumuiya hiyo ni kuunganisha nguvu kati yao na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuona kwamba uwepo wao nje ya Zanzibar unaleta faida kwa Jamii yote. Alisema hivi sasa wanakamilisha taratibu za kuwaunganisha wenzao wa miji tofauti ili ifikapo Januari mwakani Jumuiya yao ianze kazi rasmi.
“ Tumefanya utafiti na kugundua Wapo Wazanzibari wengi wenye sifa na uwezo mkubwa kitaaluma ambao wanaweza kuitumia na kusaidia nyumbani ”. Alisema Dr. Omar.
Alisisitiza kwamba taratibu zinaandaliwa za akuwaunganisha Wazanzibari wengi walioko katika Jumuiya za Uingereza na Canada kwa ania ya kuwa na kiungo muhimu kati yao na Zanzibar hasa katika maeneo ya Uwekezaji na Uatafiti katika Sekta tafauti.
Alisema kuanzishwa kwa mawasiliano ya moja kwa moja yatatoa fursa kwa wenye nia ya kusaidia kupitia jumuiya hiyo. Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza azma yan Jumuiya hiyo ya Zanzibar Diascora Organization na kuahidi kuipa Baraka.
Balozi Seif alisema Serikali inaunga mkono vikundi vya Diascora na kuvitaka kuwa karibu na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania.
“ Serikali ya SMZ tayari imeshaundan Idara inayosimamia Diascora kwa lengo la kuwaunganisha wazawa walioko nje ya Nchi. Hivyo tutahakikisha mnakuwa na mawasiliano ya karibu na Taasisi hii “ Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Othmana Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Friday, November 4, 2011

Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wanajumuiya ya Afrika ya Mashariki waishio Marekani

Wana Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoishi Florida Nchini Marekani wameombwa kuendelea kushirikiana pamoja kwa lengo la kutatua matatizo wakati yanapotokea na kuwazunguuka.
Ombi hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mjini Tallahassee Jimbo la Florida Nchini Marekani baada ya kushiriki katika chakula cha pamoja na Wana Jumuiya hao.
Balozi Seif alisema matatizo mengi yanayowakabili wanaadamu yanashindwa kupatiwa ufumbuzi kutokana na kukosekana kwa ushirikiano wa pamoja.
“ Wana Jumuiya nyinyi ni vyema mkapendana na kushirikiana kwa vile mko mbali na familia zenu mnazozitegemea. ”. Alisema Balozi Seif Al Idi.
Amewataka kufuata Sheria na taratibu zilizowekwa Nchini humo ili kuepuka adhabu inayoweza kuwaletea balaa katika mfumo wa maisha yao ya kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amewapongeza wana jumuiya hao wa Afrika Mashariki wanaoishi Florida Marekani kwa uwamuzi wao wa kuunda umoja wao unaosaidia kusukuma mbele maisha na Maendeleo yao.
Hata hivyo amewakumbusha hatma ya maisha yao ya baadaye ambayo inahitaji kufanyiwa maandalizi ya msingi.
Balozi Seif alisema haipendezi kuona mwana Jumuiya anafanya kazi ughaibuni lakini hatma ya maisha yake arudipo nyumbani inavunja moyo.
“ Inakua karaha unarudi ughaibuni na kutaka kuishi kwenye nyumba ya mjomba. Huko ni kujidhalilisha na kujimaliza kimaisha ”. Alitahadhaisha Balozi Seif Ali Iddi.
Umoja wa Wanajumiya ya Afrika Mashariki ulioanzishwa karibu miaka saba iliyopita Umejumuisha pia Wanachama kutoka Mataifa ya Carribean na Nigeria.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yassaini mkataba wa mashirikiano katia yake na chuo cha ufundi cha Florida

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba wa Mashirikiana kati yake na Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida { FAMUJ } Nchini marekani.
Mkataba huo una lengo la kubadilishana uzoefu na Utaalamu kati ya chuo hicho na chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZAZ}.
Utiaji saini huo umefanyika katika Majengo ya Chuo hichocha Florida yaliyopo katika mji wa Tallahassee ambapo kwa upande wa Zanzibar umewakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Florida umewakilishwa na Rais wa Chuo hicho cha
{ FAMU } Dr. James ammons.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa pia na wanafunzi wa fani fofauti chuoni hapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri taaluma inayotolewa na chuo kikuu cha Florida iingie katika nchi changa ili kuleta mabadiliko ya kilimo na ufundi.
Balozi Seif alisema Mataifa mengi yanayoendelea hasa yale ya Bara la Afrika bado yanashindwa kukabiliana na changamoto zinayoyabaliki licha ya kwamba Mataifa hayo yanategemea Kilimo kwa asilimia zaidi ya 70%.
“ Florida University iwe kiungo cha kuunganisha Taaluma katika vyuo vikuu vya nchi changa kikiwemo kile cha suza ”. Alisema Balozi Seif.
Mapema Rais wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida
{ famu } Dr.James Ammons alisema Chuo hicho kinalenga kujenga nguvu ya Taaluma katika kuona kizazi cha sasa kinapata Elimu inayokwenda sambamba na mabadiliko ya kasi ya Sayansi na Teknolojia Duniani.
Dr. ammons alisema Chuo hicho kilichoanzishwa miaka 125 iliyopita kimefungua masomo ya Taaluma ya Madawa na Sheria yakianguliwa nay ale ya Kilimo na Ufundi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata fursa ya kukitembelea kitengo cha Ufundi cha Chuo hicho cha Florida
{ FAMU -FSU }.
Mkuu wa Kitengom hicho cha ufundi Dr. Regional Perry alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake hatua waliyofikia chuoni hapo ya kifanya utafiti katika masuala ya Madawa na Wanaadamu.
Dr. Perry alisema wataalamu wa chuo hicho tayari wamefikia hatua ya kutengeneza Injini za vyombo vya moto.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Balozi Seif Ali Iddi

Mwakilishi wa Bara la Afrika katika Umoja wa Mataifa Balozi Amina Salim Ali amewataka Watanzania kulitumia vyema soko la Marekani katika kukuza uchumi wa Taifa.
Balozi Amina alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake ulipomtembelea Ofisini kwake Mjini Washington DC Nchini Marekani.
Amesema Marekani kupitia mashirika na makampuni kadhaa ya Nchi hiyo hivi sasa yameelekeza nguvu katika kuwekeza Vitega Uchumi kwenye Mataifa kadhaa Ulimwenguni.
“ Hakikisheni Watanzania mnachangamkia vyema fursa hizo ambazo wenzetu wa Nigeria, Ethiopia na hata Majirani zetu wa Kenya wanazitumia ”.Alisema Balozi Seif.
Balozi Amina ameziasa taasisi zinazosimamia uwekezaji kuwa makini na wawekezaji wanaoonyesha hamu ya kutaka kuwekeza.
Amesema si vyema kwa wawekezaji hao kuhangaishwa wakati wanapotaka kuwekeza vitega uchumi vyao Nchini.
Balozi Amina ameupongeza Ujumbe huo wa Zanzibar unaofanya ziara Nchini Marekani kwa hatua yake ya kuitangaza Zanzibar kwa wawekezaji wa Marekani kufungua milango ya uwekezaji Zanzibar.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi alimshukuru Balozi Amina kwa kuwa kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya Zanzibar na Wawekezaji wa Marekani.
Balozi Seif alisema Mwakilishi huyo wa Bara la Afrika katika Umoja wa Mataifa amechangia kuifanya ziara hiyo kuwa ya mafanikio kwa kiwango kikubwa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Utafiti wa mradi wa samaki Zanzibar na Marekani

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Taasisi ya Ushirikano ya Jimbo la Houston,Texas Nchini Marekani zimefikia hatua ya kukubaliana kufanya utafiti wa pamoja utakaopelekea kuanzishwa kwa Mradi mkubwa wa Samaki Zanzibar.
Hatua hiyo ya makubaliano imekuja kufuatia Kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Zanzibar ulioko Nchini Marekani Kujitanga kwa wawekezaji wa Nchi hiyo ukiongoza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Taasisi inayoratibu Miradi mikubwa ya Samaki Nchini Marekani ya { GRI } ikiongozwa na Rais wa soko la Kimataifa la Taasisi hiyo Bwana Tomas Newland.
Mazungumzo hayo yamefanyika hapo katika Afisi za Taasisi hiyo kwenye Jimbo la Houston, Texas Nchini Marekani.
Bwana Tomas Newland aliueleza ujumbe huo wa Zanzibar kwamba mradi huo mkubwa una uwezo wa kutoa ajira kwa Wananchi zaidi ya thalathini elfu.
Alisema miradi kama hiyo ambayo tayari imeshaanzishwa katika baadhi ya Mtaifa ya Afrika,Asia, Marekani na Ulaya inazingatia zaidi uhifadhi wa Mazingira pamoja na utoaji wa mafunzo kwa Wavuvi na Wakulima wa maeneo ya Vijijini.
“ Miradi kama hii ambayo hufadhiliwa na Taasisi za Uwekezaji Vitega Uchumi za OPIC na IFC hugharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 20,000,000.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri kuharakishwa kwa mawasiliano ya pamoja kati ya wataalamu wa pande hizo mbili ili kuona wazo hilo la muelekeo wa kuanzishwa kwa mradi mkubwa wa Samaki linafanikiwa.
Balozi Seif alisema kuanzishwa kwa mradi huo mbali ya kuleta uhusiano wa karibu kati ya Zanzibar na Marekani lakini pia utaleta faraja kwa Wananchi walio wengi kujipatia ajira ya uhakika.
Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikuwa na mazungumzo na Seneta wa Jimbo la Houston,Texas Bwana Rodey Ellis.
Katika mazungumzo yao Senata Rodney aliiponhgeza Zanzibar kwa juhudi zake za kharaisha Maendeleo ya Kiuchumi.
Seneta Rodney Ellis amemkabidhi Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake hati Maalum inayompa heshima ya kuwa mkaazi wa Jimbo la Houston, Texas.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Zanzibar yashuriwa kulitumia vizuri soka la Afrika ya Mashariki

Zanzibar imeshauriwa kulitumia vyema soko la Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Mashariki kwa lengo la kukuza uchumi wake na kuondokana na kutegemea zao moja la karafuu kama mhimili wa Taifa.
Ushauri huo umetolewa na Mkamu wa Rais wa Shirika la uwekezaji Vitega Uchumi la Kimataifa Nchini Marekani { OPIC } Bibi Mimi Alemahou wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Washington DC Nchini Marekani.
Bibi Mimi alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake ulioko nchini Marekani kwa ziara ya Kikazi ya
kuitangaza Zanzibar kwa wekezaji kuwekeza Zanzibar kwamba Shirika hilo tayari limeshaandaa mpango wa kuwekeza ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki likilenga kusaidia eneo hilo Kiuchumi.
Alisema mpango huo una nia pia ya kuijumuisha Sudan ambayo imekuwa ikikabiliwa na ukame wa mara kwa mara licha ya kwamba haimo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki { EAC }.
“ Tumelenga zaidi kuisaidia Sekta Binafsi kwa vile jamii kubwa hasa ndani ya Bara la Afrika imekuwa ikikabiliwa na Uchumi duni ”. Alisema Bibi Mimi Alemayehou.
Bibi Mimi alifahamisha kwamba huduma za Shirika hilo la OPIC mara kahaa huelekezwa katika kutoa huduma za Kijamii kwenye sekta Binafsi kupitia Makampuni ya Kimarekani Chini ya Shirika la Misaada la Marekani US aid.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi ameuambia Uongozi wa Shirika hilo la Uwekezaji Vitega Uchumi la OPIC kwamba Zanzibar bado inaendelea kutegemea zao moja tu la Uchumi la akARAFUU.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko katika harakati za kuimarisha miundombinu ili kuyawezesha Makampuni ya Kigeni kupata fursa ya kuwekeza Zanzibar.
Alisema wawekezaji katika Sekta ya Utalii wana nafasi nzuri ya uwekezaji kwa vile miundo mbinu ya bara bara, maji na umeme iko katika hatua nzuri.
Hata hivyo Balozi Seif ameuomba Uongozi wa OPIC kuangalia uwezekano wa kuanzisha mradi wa pamoja wa umeme kwa kutumia Nishati ya jua au Bahari ili Zanzibar iwe tayari kukabiliana na upungufu wa huduma ya umeme hasa wakati kinapopungua kina cha maji huko Tanzania Bara.
“ Tumekuwa tukipokea huduma ya umeme kupitia Gridi ya Taifa huko Tanzania Bara, lakini wakati mwengine tunalazimika kupata umeme wa mgao kutokana na kupungua kwa kina cha maji. Hali hii huathiri utendaji kazi na kupunguza kasi ya Maendeleo ya Kiuchumi ”. Alisema Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Balozi Seif.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Thursday, November 3, 2011

Sanaa na wasanii

Mwambiji Amina wa Kikundi cha taarabu cha cluture