Thursday, August 25, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UCHUMI WA KIBEPARI CHANZO CHA MGOGORO WA MAFUTA
Kutangazwa punguzo la bei mpya za nishati ya mafuta tarehe 3/08/2011 na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati (EWURA), ilipelekea makampuni ya mafuta kufanya mgomo baridi wa kutouza mafuta kwa siku kadhaa. Jambo lililowatia dhiki na mashaka raia na kudhoofisha maisha ya kijamii na kiuchumi, na hatimae EWURA kusitisha leseni ya kampuni ya BP kuuza mafuta kwa jumla kwa miezi mitatu, kampuni ambayo serikali inamiliki nusu ya hisa, na pia EWURA kuzionya kampuni nyengine za Camel na Engen.
Kwa kadhia hii, Hizb ut-Tahrir Afrika ya Mashariki ina haya ya kusema: Chanzo cha mgogoro huu ni upotofu wa nidhamu ya kiuchumi ya kibepari ambayo imechanganyikiwa ambako hudhihirika katika mambo matatu: Kwanza, kwa ajili ya maslahi haitofautishi baina ya ‘mali za binafsi’ na ‘mali ambazo ni za umma’ kimaumbile. Pili, utozaji wa makodi makubwa katika biashara, na mwisho unafiki wa dhana ya ‘soko huria’.
Nidhamu bora na tukufu ya kiuchumi ya kiislamu ambayo Hizb ut-Tahrir Afrika ya Mashariki inaamini kuwa ndio suluhisho pekee, imeweka mpaka wa wazi katika mafungu ya mali, kwa kuanisha ‘mali binafsi’ zinazoruhusiwa mtu yoyote kumiliki, ‘mali za serikali’ zinazofanana na mali binafsi isipokuwa tu humilikiwa na serikali kwa sababu ya kuhusika na haki ya jamii na ‘mali za umma’ ambazo huwa marufuku kumilikiwa na mtu binafsi kwa hali yoyote ile. Mali za umma kimaumbile ni za watu wote, kama vile mali zote za asili- migodi mikubwa ya maadini, fukwe, misitu, barabara na kila ambacho maumbile yake ni cha matumizi ya umma kwa ujumla wake. Mali hizi na mfano wa hizi huwa kamwe hazimilikiwi na mtu binafsi, taasisi au kikundi cha watu, kwa kuwa raia wataingizwa katika dhiki na mashaka kama haya yaliyojiri karibuni na yatakayoendelea kujiri chini ya mfumo huu. Pia hizi si mali za serikali kama ilivyo ndani ya mfumo potofu wa Ukomunisti, bali kazi ya serikali ni kuzisimamia tu na kuwafikishia umma kwa namna nyepesi ya haraka na muafaka. Mtume (SAW) alizuia kummilikisha Abyadh bin Hammal mgodi mkubwa wa chumvi, na pia anasema: “Watu ni washirika katika mambo matatu: maji, maeneo ya kulishia wanyama na moto.” Hapa ‘moto’ huhusisha kila aina ya nishati. Pia Uislamu ukaweka bayana kwamba kazi ya serikali ni kuwatumikia raia kama msimamizi na sio tu kutoza makodi, bali serikali nayo ijihusishe kuzalisha kwa kufanya biashara mbalimbali kama raia wengine. Na tatu, katika Uislamu hakuna unafiki wa kuchanganyikiwa kama ulivyo ubepari ambao asili yake huwapa mamlaka makubwa mabepari kuwanyonya wanyonge kwa dhana yao ya ‘soko huria’ na upande wa pili hujifanya ati una huruma kwa kupachika kiraka kinachogongana na mfumo wao kwa madai ya kiuwongo ya ati kuwasaidia wanyonge kwa kupanga baadhi ya bei za bidhaa muhimu! Ama Uislamu, ukiachilia mbali mali za umma na mali za serikali, mali zilizobakia zote ni haki ya raia wenyewe kupanga bei zao bila ya kuingiliwa, na hili pia huhusisha bei za huduma na mishahara kwa kuwa suala la kazi ni mkataba baina ya muajiri na muajiriwa peke yao. Na pale ambapo raia kapungukiwa katika kukidhi mahitaji yake ya msingi huwa ni jukumu la serikali (Khilafah) kumkidhia raia huyo mahitaji yake.
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inatangaza wazi kwamba kadhia hii ni dhihirisho nyongeza kwamba dunia leo inahitaji nidhamu mbadala ya kiuchumi kama inavyohitaji nidhamu mbadala ya kisiasa na kijamii ili kuokoa ubinaadamu, nidhamu ambayo ni ya kiislamu na sio nidhamu ya kibepari inayowatia watu dhiki na iliyosheheni viraka vinavyogongana na misingi ya mfumo wake.
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HIZB UT- TAHRIR AFRIKA MASHARIKI YAWASILISHA ‘SHUTUMA YA DHULMA DHIDI YA WAISLAMU’ KWA UBALOZI WA PAKISTAN
Tarehe 12/08/2011 Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki iliwasilisha rasmi shutma kwa ubalozi wa Pakistan jijini Dar-es-Salaam dhidi ya vitendo vya nchi hiyo vya dhulma, maonevu na unyakuzi wa kuwatia nguvuni kisiri wanaharakati wa Kiislamu wasio na hatia, kwa ‘kosa’ tu la kuulingania Uislamu kifikra bila ya kujihusisha na kitendo chochote cha nguvu.
Shutuma hizo ziliwasilishwa na Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki (Masoud Msellem) na Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano ya Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki (Sheikh Mussa Kileo), na kukabidhiwa Afisa Utawala na Mwambata wa ubalozi wa Pakistan nchini Tanzania bwana Masud Hassan Khan. Pamoja na shutma hizo Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki iliwasilisha pia waraka maalum uliotolewa na Hizb ut-Tahrir ndani ya Pakistan, unaotaja kinaga ubaga majina na mazingira ya unyakuzi wa Naibu msemaji wa Hizb ut-Tahrir Pakistan (Imran Yousafzai) na wanachama wengine waandamizi wa Hizb ut-Tahrir ndani ya Pakistan akiwemo Hayan Khan, Ousama Hanif na Dk. Abdul-Qayuum. Wote walinyakuliwa kisiri na wanaendelea kushikiliwa mafichoni pa siri kwa dhulma na serikali ya Pakistan bila ya hatia yoyote. Aidha Hizb ut-Tahrir Afrika ya Mashariki iliisisitiza (demand) serikali ya nchi hiyo kuwacha vitendo hivyo vya dhulma mara moja na kuwaachia huru Waislamu hao. Shutuma kama hizi pia ziliwasilishwa kwa ubalozi wa Pakistan jijini Nairobi kwa kupitia Mwakilishi wa Vyombo vya Habari wa Hizb ut-Tahrir Afrika ya Mashariki (Shabani Mwalimu)
Licha ya Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki kulaani kwa nguvu zote dhulma na uonevu huu na kuwataka Waislamu wote na kila mwenye chembe ya ubinaadamu kulaani unyama huu na kufanya upeo wa jitihada ili wahanga waachiwe huru. Pia tunatangaza kwa sauti ya juu kwamba dhulma na mateso hayawezi kamwe kuzuia Hizb kuendelea na kazi yake tukufu ya kulingania Uislamu kama mfumo bora mbadala hadi hatima ya kuasisi serikali yake, Khilafah Rashidah katika nchi kubwa za kiislamu kama ilivyobashiriwa na Allah Ta’ala na Mtume Wake (SAAW), ili kuukomboa ulimwengu mzima na uovu wa mfumo wa kibepari ukiwemo kukamata na kutesa watu kwa kutangaza haki. Siku hiyo, madhalimu watajuta lakini majuto yao hayatuwasaidia chochote!
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

Melbourne Unveils Draft Plan to Strengthen Business Ties with India, IST

The Australian city of Melbourne has announced a draft plan to strengthen business ties with India, with a focus on building economic prosperity, facilitating learning and supporting community, cultural and civic links between the two countries. The city of Melbourne already has a strong working relationship with India and this engagement framework will ensure it continues to grow. Currently, India is Australia's fifth largest trading partner and through this engagement, the city of Melbourne now plans to focus on three key goals -- building economic prosperity, facilitating learning and supporting community, cultural and civic links between the countries

Gems, Jewellery Exports Grow 5.4% in July, PTI
Gems and jewellery exports grew at a slow pace of 5.4 per cent to USD 3.3 billion in July year-on-year. In the previous month, the exports had jumped by 17 per cent. The exports stood at USD 3.1 billion in July last fiscal. The US accounts for about 25 per cent of the country's total gems and jewellery exports, Europe contributes 20 per cent. demand from new markets like Russia, Latin America and Africa is increasing

Monday, August 22, 2011

Afrika kusini yakana kumtorosha Gadhafi

Afrika Kusini imesema haijatuma ndege Libya kumsaidia kiongozi wa nchi hiyo anayepingwa Moammar Gadhafi ili kuondoka nchini.
Katika taarifa yake jumatatu, Serikali ya Afrika Kusini imesema inataka kukanusha tuhuma kwamba ndege za Afrika Kusini zitamsafirisha kanali Gadhafi na familia yake kwenda sehemu isiyojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje Maite Nkoana –Mashabane alisema bwana Gadhafi hajaomba hifadhi Afrika Kusini na anauhakika kwamba hawezi kufanya hivyo. Amsema haijulikani mahali alipo kiongozi wa Libya.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliongoza juhudi za umoja wa Afrika kutatua mzozo wa Libya baina ya Serikali ya bwana Gadhafi na waasi wanoungwa mkono na magharibi.
Huku ikionekana kuwa bwana Gadhafi ataanguka, Afrika Kusini imesema jumatatu kwamba inaunga mkono utaratibu wa Umoja wa Afrika unaotaka kuwepo serikali ya mpito ya Libya, kuandika rasimu ya katiba mpya, na kuitishwa kwa uchaguzi wa kwanza kabisa wa kidemokrasia nchini humo

Kura ya maoni Liberia

Wananchi wa Liberia wanatarajiwa kwenda kupiga kura siku Jumanne kwa ajili ya kutoa mapendekezo yao ya mabadiliko ya katiba ambayo yanaungwa mkono na chama tawala wakati huo huo chama cha upinzani nchini humu wanapingwa vikali mabadiliko hayo.

katika hali hiyo wabi mojawapo ya mabadiliko makubwa ambayo yanaonekana kuwa na nchini Liberia ni ile nafasi ya ugombea wa kiti cha urais ambapo kwa ujibu wa sheriza nchini hiyo, mtu anayetaka kugombea nafsi hiyo, anatakiwa awe ameishi nchini Liberia kutoka miaka 10 hadi 5.

Hali hiyo inaonekana inaweza kuathiri harakati zakisiasi nchini humo, kwani sheria inatakiwa iweseme ni wagombea gani wanaostahili kushiriki katika kinganganyri cha uchaguzi ujao. Wanasiasa wengi ambo waliondoka nchini humo wakati wa miaka 14 uhamishoni, hii ni kutokana na ghasia na machafuku za kiraia ambayo yalikuwa yakitokea nchini humo na kumalizika mwaka 2003.

Mabadiliko mengine yatachelewesha uchaguzi wa rais kutoka Oktoba mpaka Novemba.Waungaji mkono wanasema hatua hiyo itauondoa uchaguzi wakati wa msimu wa mvua ambapo usafiri unakuwa mgumu sana

Waasi waiteka Tripoli

Maelfu ya wakazi wa Tripoli wamekuwa wakisherehekea usiku kucha wakati wapiganaji walipoingia katika uwanja mashuhuri ambao wameubadilisha jina lake mara moja na kuitwa uwanja wa mashujaa ambako wa Libya waliokuwa na furaha walianza kuangusha na kuharibu mabango makubwa ya picha ya bwana Gadhafi na kuanza kuyakanyaga.
Hadi hivi karibuni serikali ya Libya imekuwa ikiutumia uwanja huo kuanda maandamano makubwa ya wananchi kuonesha uungaji mkono wa kiongozi wa Libya ambaye anaonekana kuwa ameshindwa hivi sasa.
Viongozi wa upinzani hata hivyo wamekiri alfajiri ya Jumatatu kwamba kungali kuna maeneo ambayo kuna upinzani ndani na nje ya Tripoli. Msemaji wa upinzani amesema wapiganaji wameshauzingira uwanja wa Bab Alazizya ambako wanaamini huwenda bwana Gadhafi amejificha lakini wanasita kuanza kushambulia.
Msemaji wa waasi anasema walipeleka kundi la wapiganaji kuingia katika mji mkuu kupitia bahari kutokea bandari ya Misrata. Aliongeza kusema kwamba kikosi maalum cha ulinzi wa Gadhafi kimejisalimisha na hivyo kuwawezesha wapiganaji kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya mji

Sunday, August 21, 2011

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitosita kuwachukuliwa hatua za kisheria muda si mrefu viongozi wote waliohusika na masuala ya uvushaji wa magendo ya zao la karafuu nje ya Nchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Mabalozi wa CCM wa Mashina yaliyomo ndani ya Wadi ya Fujoni hapo Afisi ya CCM Tawi la Fujoni Wilaya ya Kaskazini B.
Balozi Seif amesema Viongozi waliohusika na Biashara hiyo ya Magendo ya Karafuu wanajuilikana na hatua ya kuwachukula sheria ina lengo la Kulinda Heshima ya Serikali. Amesema uamuzi wa Serikali wa kupandisha bei ni kuimarisha pamoja na kushajiisha uzalishaji wa zao hilo ambalo ni uchumi na muhimili wa Uchumi wa Taifa. “Hakuna sababu tena ya zao la Karafuu kuuzwa nje ya Nchi Kimagendo kwa vile bei ya bidhaa hiyo imepandishwa kuzingatia soko la Dunia ” . Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Amewaomba wakulima kuzidi kuimarisha kwa wingi uzalishaji wa mikarafuu mipya kwa lengo la kujiongezea kipato chao na kupunguza makali ya maisha. Akizungumzia suala la uchaguzi wa Viongozi wa CCM utakaofanyika Hapo mwakani Balozi Seif ambae pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM amewatahadharisha Mabalozi hao kuwa makini katika kuepuka tabia ya kutanguliza ujomba katika kuchagua Viongozi.
Balozi Seif amesema ni vyema ikaeleweka kwamba wanayemchagua anafaa kuwaongoza akiwa na vigezo vyote vya uongozi. Amesisitiza kwamba Tabia ya kuendeleza urafiki katika suala la uongozi inapunguza sana nguvu za chama. Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kitope amemaliza ziara yake ya kukutana na Mbalozi wa Mashina ndani ya Jimbo hili
Othman khamis ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Saturday, August 20, 2011

Press release

Wawekezaji wa Uingereza bado wana nafasi ya kuwekeza ndani ya Visiwa vya Zanzibar katika sekta ya viwanda kwa lengo la kusaidia suala la ajira hasa kwa vijana . Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo wakati akihojiwa na Mwandishi wa Gazeti la World Report lenye makao yake Makuu Mjini London Nchini Uingereza Bibi Barbara Yankovic.
Balozi Seif Ali Iddi amesema uamuzi wa Wawekezaji wa nchi hiyo kuwekeza katika eneo hilo la Viwanda ambalo linachukuwa ajira kubwa zaidi bado liko finyu katika Uwekezaji. Amesema Changamoto kubwa inayoikabili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa ni suala la ajira. Hivyo juhudi zinaendelea kuchukuliwa ili kuona eneo hilo linapata ufanisi katika kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira. “ Uingereza na Zanzibar zina Historia ndefu sana katika masuala ya Kibiashara. Hivyo nafasi hiyo itasaidia kuimarisha zaidi ukaribu huo ” Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif amemueleza Mwandishi huyo kwamba miundo mbinu katika sekta nyengine kama vile Afya, Elimu, Utalii na Kilimo imefikia kiwango cha kuridhisha. Amesema kinachozingatiwa kwa sasa ni kuongeza nguvu zaidi katika sekta ya kilimo kwa vile inachukuwa asilimia 70% ya watu wote wa Zanzibar wanaoishi vijijini. Kampuni Binafsi inayomiliki Gazeti la World Report imekuwa ikichapisha makala na kutangaza mambo ya Kiuchumi, Wafanyabiashara na Uwekezaji hasa katika Sekta za Utalii . Hatua hiyo ina lengo la kuwashajiisha Wawekezaji tofauti wa Kimataifa kuwekeza katika Mataifa ambayo tayari yanasimamia vyema amani na kufuata utawala wa kidemokrasia.
Waandishi wa Gazeti hilo la World Report tayari wameshakutana na viongozi wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar pamoja na Taasisi ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } kwa mazungumzo na kuangalia mazingira ya kuyatangaza maeneo hayo kwa wawekezaji nje ya nchi.
Gazeti hilo tayari limeshafanya utafiti wa Utawala Bora na kutangaza mambo ya Kiuchumi na Uwekezaji katika Mataifa ya Cameroun, Angola pamoja na Tanzania Bara.
Othman Khamis
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Thursday, August 18, 2011

kutatua migogoro kwa njia ya amani

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishauri jamii kuendeleza utamaduni ya kutatua migogoro inayowazunguuka kwa njia na majadiliano ili kuepuka unyakuzi wa haki na maisha ya wananchi. Amesema majadiliano yanaondoa matumizi mabaya ya silala, uhasama na hatimaye kuepusha shari inayoweza kuzaa maafa.
Balozi Seif amesema hayo baada ya kuangalia eneo huru la kiuchumi lililoleta mgogoro baina ya vijiji vya wingi na maziwang'ombe micheweni Pemba na kupelekea Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni Kuunda tume ya kusuluhisha mgogoro huo kwa njia ya majadiliano. Akizungumza na Viongozi wa Tume hiyo hapo Skuli ya Micheweni Balozi Seif amesema uwamuzi wa pamoja wa majadiliano kati ya pande hizo mbili umeleta faraja kwa Serikali na kupelekea wananchi wa eneo hilo kuishi kwa raha na amani.
Ameupongeza uwamuzi huo ambao hata Jumuiya ya Kimataifa zinautumia katika kutafuta suluhu za matatizo mbali mbali yanayotokea baina ya jamii au mataifa tofauti. ''Tungeendelea na vurugu za kukaribisha kutumika kwa marungu na mapanga tusingefikia hatua hii iliyoleta faraja kwetu sisi hasa viongozi wa ngazi za juu wa serikali'' Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Amewapongeza wananchi wa Wingwi na Maziwa ngo'mbe kufikia hatua hii ya amani na kuvishauri vijiji vyengine kuiga mfano huu. Amesema bado ipo migogoro kama hii kwa baadhi ya vijiji hapa nchini na cha kuzingatia ni kuona hatua ya mafakiano inafikiwa kwa kutumia tume za majadiliano baina ya pande zinazohusika na mgogoro.Mapema Mkuu Wilaya ya Micheweni nd. Juma Abdulla amesema eneo hilo la maeneo huru ya serikali ambalo lieasisiwa tokea mwaka 1992 linawapa fursa wananchi wa maeneo hayo kulitumia kwa vipando vidogo vidogo vya muda hadi hapo serikali kuu itapokuwa tayari kuwekeza. Nd. Juma amesema tamaa ya baadhi ya watu kuhodhi ardhi bila ya kuzingatia taratibu zilizopo ndio inayopelekea kuleta migogoro ya ardhi

Tangazo la mkutano mkuu wa MISA

TAASISI YA VYOMBO VYA HABARI KUSINI MWA AFRIKA–TAWI LA TANZANIA (MISA-TAN) INAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA WAKE KUHUSU MKUTANO MKUU WA MWAKA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA ASASI HIYO. MKUTANO HUO UTAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA RUSSIAN CULTURAL CENTRE, UPANGA SEA VIEW, SIKU YA JUMAMOSI SEPTEMBA 10, 2011 KUANZIA SAA 3.00 ASUBUHI
AGENDA
1. Ufunguzi na Kuhakikisha “quorum”
2. Kuridhia Ajenda
3. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita
4. Yatokanayo
5. Kuwasilisha na Kupitisha Ripoti ya Mwaka 2010/2011
6. Kuwasilisha na Kupitisha Ripoti ya hesabu za Mwaka 2010/2011
7. Uchaguzi wa Viongozi
8. Mengineyo
9. Kufunga mkutano
Wanachama wote hai wanakaribishwa kuhudhuria.
Wale wote wanaotaka fomu za kugombea uongozi katika Baraza la Uongozi la Taifa (NGC) kwa mujibu wa katiba ya MISA-Tan wanatakiwa kuchukua na kurudisha fomu hizo kabla ya tarehe 2 Septemba 2011. Ofisi ya MISA-Tan haitapokea fomu yoyote baada ya tarehe hiyo. Nafasi za kugombewa ni pamoja na Mwenyekiti, Mjumbe mmoja mwenye taaluma ya sheria, Mwekahazina ambaye atakuwa na sifa za uhasibu na wajumbe sita wa NGC. Wajumbe hao sita watachaguliwa kulingana na kanda (kama Katiba ya MISA-Tan ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2007). Kanda hizo ni Zanzibar,Kanda ya Mashariki (DSM, Morogoro, Pwani, Mtwara na Lindi),Kanda ya nyanda za Juu Kusini (Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma), Kanda ya Ziwa (Shinyanga, Kagera, Mwanza, Mara na Kigoma) Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Tabora) na Kanda ya Kaskazini (Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga). Wagombea wote na wapiga kura wanatakiwa kuwa wanachama kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.
Ukisoma tangazo hili mtaarifu na mwenzako
NB: FOMU ZIWASILISHWE OFISINI KWETU CLOCKTOWER SHOPPING CENTRE GHOROFA YA KWANZA CHUMBA NAMBA 2 , MTAA WA UHURU/NKRUMAH AMA KWA BARUA PEPE.
IMETOLEWA NA
ANDREW MARAWITI
KAIMU MKURUGENZI

Tuesday, August 16, 2011

Waziri wa Miundu mbinu na mawasiliano wa Zanzibar akipokea msaada wa TV kutoka kwa kamapuni ya simu za mikononi ya Zantel, TV hiyo itatumika airport






Karafuu Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepongezwa kwa juhudi zake inazochukuwa katika kuhakikisha Zao la Taifa la Karafuu linauzwa katika Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar { ZSTC }. Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya Mabalozi wa wadi ya Kitope wakati wa kikao chao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Ofisi ya Jimbo hilo iliyopo Kinduni .

Mabalozi hao wamesema udhibiti mzuri wa zao hilo pamoja na Bei muwafaka umepelekea Wakulima wa zao hilo kuuza Bidhaa hiyo katika Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar { ZSTC }.Wamesema kiwango kikubwa cha ununuzi wa zao hilo katika kipindi kifupi cha msimu huu kinaashiria mkakati madhubuti uliowekwa na Serikali wa udhibiti wa zao hilo kupitia kamati za Ulinzi, Masheha na Wananchi.

“Nimesikia leo katika Vyombo vya Habari huko Pemba kwamba Tani zisizopungua mia moja zimeuzwa ZSTC . Kwa hilo linastahiki kupongezwa ” Amesema mmoja wa Mabalozi hao Bwana Makame Ali Mussa. Akizungumza na Mabalozi hao wa Wadi ya Kitope Balozi Seif Ali Iddi amewasisitiza kuendeleza Umoja wao wakati wote kwa lengo la kufanikisha Malengo waliyojipangia. Balozi Seif amewanasihi Viongozi hao kujitokeza kugombea nafasi tofauti wakati utakapowadia uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi.

Wakati huo huo Balozi Seif Ali Iddi amekabidhi jumla ya Shilingi Milioni Mbili na laki nne kutunisha Mfuko wa Maendeleo wa Jumuiya wa Wastaafu wa Taasisi za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Fedha hizo zimetolewa na Baadhi ya waheshimiwa Wawakilishi na Mbunge wa kikwajuni zimekuswanywa chini ya dhamana ya Balozi Seif kufuatia mchango wa papo kwa papo iliyofanywa tarehe 11 juni mwaka huu.

Akizungumza na Wastaafu hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amesema Jumuiya kama hii kujikusanya katika kujitafutia ajira ni jambo la msingi na huleta Heshima kwao. Amesema huo ni mfano mzuri kwa vile hawakujibweteka katika kujitafutia maisha, hivyo ni vyema kwa wastaafu wa Taasisi za Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar kuiga mfano kama huo. Naye mlezi wa Jumuiya hiyo Bibi Tereza Olban Ali amempongeza Balozi Seif kwa jukumu alilolikubali ambalo limeleta faraja kwao.

Waheshimiwa waliochangia mchango huo ni Mwenyewe Balozi Seif Shilingi Milioni 1,000,000/- ,Mwakilishi wa jimbo la Rahaleo Mh. Nassor Jazira Shilingi laki 700,000/- na Mwakilishi wa jimbo la Amani Mh. Fatma Mbarouk Shilingi laki 350,000/- Wengine ni Naibu Waziri wa Habari Mh. Hindi Hamad Shilingi laki 150,000/-, Mwakilishi wa jimbo la Kikwajuni Mh. Mahmoud Mohd Shilingi 100,000/- na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuini Mh. Masauni Yussuf Masauni Shilingi 100,000/-.

Wednesday, August 10, 2011

Mtegani Fm watembelewa na UN Women kutoka Dar

Muwezeshaji kutoka UN Women Organization Bi Rose Haji mwenye kipaza suti akizungumza machache wakati alipotembelea Mtegani Fm radio Mkundunduchi

Mratibu wa UN Women mwenye kipaza sauti Bi Salome Wanyote akiwa na wajumbe wenzio kutoka Dar mara walipotembelea katika kituo cha radio cha Mtegani-Makunduchi Zanzibar

Bi Salome wa Nyote na Bi Rose Haji wakiwa pamoja kwenye kitua cha radio cha Mtegani Fm radio Makunduchi wilaya ya kusini Unguja


Mtangazi wa Mtegani Fm radio akiwa katika kipindi

Friday, August 5, 2011

Dhahabu Ghana

Unga wa dhahabu au ni vumbi la dhahabu?



Hii vivyo vinoo vya dhahabu ambayo tayari imeshakwisha tayarishwa na sasa inasubiri wateja

Monday, August 1, 2011

Taaswira katika picha

Ndani ya chumba cha matangazo hits fm Zanzibar


















Mhariri wa hits fm akitowa maelezo mafupi kwa viongozi wa Lindi Press Club Program Manager wa Zenj Fm akifafanua kitu